Hivi karibuni VodaCom Tanzania ilizindua huduma ya CHEKA TIME ambapo mteja atatumia robo shilingi kwa sekunde. Hii ni huduma ya aina yake na hajawahi kutokea katika historia ya mawasiliano hapa nchini.
Kwa mantiki hiyo, VodaCom hivi sasa ndio imekuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo inatoa huduma kwa gharama nafuu ukilinganisha na kampuni nyingine nchini ambazo Watanzania walio wengi wanazimudu.
Picture
Mwamvita Makamba - Mk. Mahusiano/Mawasiliano, VodaCom(T)
Vodacom hivi karibuni pia imezindua huduma ya HABARI NDIYO HII kwa lengo la kurahisisha mawasiliano kweye familia yake na kwamba kupitia huduma hii wateja wa Vodacom wanaweza kupiga simu kwa kiwango cha shilingi moja kwa sekunde kwa masaa 20 kwa siku. Huduma hii ni Vodacom kwenda VodaCom pekee.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa VodaCom Tanzania, Mwamvita Makamba amesema kwamba wateja wa VodaCom kupitia CHEKA TIMEkwa wale wanaojisajili kwa shilingi 200 na shilingi 500 sasa wanaweza kuongea kwa chini ya robo shilingi kwa sekunde, sawa na senti 0.22 kwa sekunde.

“Hii inamaanisha kwamba Vodacom sasa ndiyo mtandao unatoa huduma kwa gharama rahisi kuliko mitandao mengine yote nchini”, amesema.

Kwa mujibu wa Bi Makamba, huduma hii itaiwezesha familia ya VodaCom kuwasiliana kwa gharama ya chini zaidi na kwamba ana imani kwamba huduma hii itachochea ukuaji wa uchumi wetu kwa maana ya Watanzania wenye shughuli mbalimbali wana uhakika wa kuwasiliana bila kikwazo chochote. Anafafanua kwamba mbali na huduma hii viwango vingine vya CHEKA TIME ya shilingi 2000 na 5000 bado vinaendelea kutumika kama kawaida.

Bi Makamba amesema kwamba huduma ya Vodajamaa nayo inaendela kama kawaida, ambayo ni mojawapo ya njia inayoiwezesha familia ya Vodacom yenye watu zaidi ya milioni saba (7) kuwasiliana kwa gharama nafuu kwa dakika na mteja anaweza kusajili watu watano kwa mara moja na watu 15 kwa mwezi mmoja. Huduma ya hii inamaanisha kwamba zaidi ya wateja milioni saba wa kampuni ya simu ya Vodacom nchini watanufaika na huduma hii mpya ya ‘HABARI NDIYO HII’ itakayokuwa endelevu na sio ya kipindi maalumi”, amesema.

Kiwango hiki cha malipo kwa watumiaji wa simu wa VodaCom Tanzania ni muendelezo wa utoaji wa huduma na promosheni zinazoambatana na zawadi mbalimbali ambazo huwafanya watumiaji wake kuwasiliana kwa urahisi.

Bi Makamba ana matumaini kwamba mabadiliko ni hakika, kuanzishwa kwake kutaboresha sekta ya mawasiliano nchini na kuwapa fursa wateja kuongea zaidi na zaidi na hivyo kuchochea shughuli mbalimbali za maendeleo kwani mawasiliano ya uhakika ni injini ya maendeleo.

“Wengi wanadhani ni jambo lisilowezekana kwamba Vodacom, ambayo inachukuliwa kuwa inatoza huduma zake kwa gharama za viwango vya juu sokoni, kuamua kutoa huduma zake kwa gharama za chini na kuweza kuendeleza nyingine”, amesema.

“VodaCom Tanzania inachukua fursa hii kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote na kuwaahidi kuendelea kutoa huduma na kuleta bidhaa zilizokuwa na ubora wa hali ya juu. Vodacom imekuwa ikitoa huduma za simu kwa muda wa miaka kumi sasa na inatarajia kukua zaidi katika sekta ya mawasiliano kwa mwaka huu na miaka ijayo”, ameongeza.

Bi Makamba alifafanua kwamba VodaCom ina shauku kubwa kwa kutoa huduma hii iliyokuwa rahisi na ya bei ya chini katika soko la wakati huu kuliko kampuni nyingine zote za simu hapa nchini. Huduma hizi za VodaCom pia ni muafaka kabisa kwa wanavikundi mbalimbali vya uzalishaji mali, wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati, wakulima, wanafunzi,wafanyakazi pamoja na wanafamilia. Kuhusu huduma nyingine kama M-PESA amesema kampuni yake inawashukuru wateja wake zaidi ya milioni mbili ambao wamesjisajili na huduma hii.

Amesema hii ni hatua muhimu lakini pia kwa mwaka huu kuna mambo mengi mazuri, mathalani kupitia huduma ya M-PESA wateja wa VodaCom kwa kutumia simu zao za mkononi hivi sasa wanaweza kulipia ankara za Umeme, maji na DSTV bila kupanga foleni lakini pia kupata huduma kwenye maduka makubwa.
Wateja wa Vodacom wanaunganishwa na Vodafone M-PESA, huduma inayotolewa kwa ushirikiano na kundi la Makampuni ya Vodafone.

Ametoa mfano wa VodaCom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya DAWASCO, imeanzisha huduma ya bure ya kulipia maji, ambapo wateja wa Vodacom Tanzania sasa wanaweza kulipia ankara zao za maji kwa kupitia simu zao za mkononi kupitia huduma ya Vodafone M-PESA.
 


Comments

Ernest
14/04/2010 21:52

In order for Vodacom to reach many more customers they would better focus on the infrastructure areas so that more people in the rural areas are able to communicate with their relatives in cities/towns. Vodacom may wish to get in touch with me for vivid examples.

Reply
bingo
14/04/2010 22:31

hii kampuni iko njema kwa kupiga porojo kwenye vyombo vya habari lakini ukiangalia ule ukweli kabisa the Cheapest network ni TIGO kwaq sababu gani? ukiangalia cost za hiyo wanayoiita cheka time lets say cheka ya sh 2000 unapewa dakika 100 wakati TIGO dakika 100 ni shilingi 1500. vile vile kama utaiangalia vizuri hii offer yao ya shilingi moja kwa sekunde haihusiki na kipindi ambacho watu wanakuwa na muda wa kupiga simu sana, katika kipindi cha jioni kuanzia saa 11 mpaka saa tatu usiku ndio matumizi ya simu yako juu na wao ndio wameweka ile bei ya kawada. kwa akili ya kawaida kama utapiga simu katika kipindi hicho cha saa 11-3 usiku ina maana ile hela inayozidi kwenye shilingi moja kwa sekunde itacompliment kwenye ile shilingi moja kwa sekunde uliyotumia mchana na kufanya Gharama kutokuwa shilingi moja kwa sekunde tena. Mi naweza kusema kwa lugha nyepesi VODACOM wana mpango waq kuwafunga midomo wateja wao kanzia saa 11jioni mpaka saa 3 usiku.

Reply



Leave a Reply