Watumishi hamsini na saba (57) wamehamishiwa katika hospitali za Dar es Salaam na thelathini na tisa (39) wamepelekwa katika hospitali za nje ya mkoa. Hospitali hiyo imepokea wafanyakazi wapya hamsini na nane (58) kutoika katika hospitali nyingine.
Kwa kuwa uhamisho siyo suluhisho pekee la kuboresha huduma katika Hospitali hiyo, Serikali imepanga kuongezewa bajeti katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha, ili kuimarisha miundombinu na vitendea kazi.
Itakumbukwa kuwa hospitali hii ya Wilaya ya Kinondoni imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu na wananchi kutokana na huduma mbovu, zisizoridhisha na kauli za kuudhi kutoka kwa baadhi ya watumishi. Malalamiko hayo yalisababisha kuundwa kwa Tume kadhaa ambazo takribani zote zilipendekeza kuhamishwa kwa baadhi ya watumishi ambao wamekuwapo eneo hilo kwa zaidi ya miaka thelathini (30) sasa.


RSS Feed