Mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Mkuchika ametoa tamko Bungeni lenye faraja kwa wanazuoni na wadau wa lugha ya Kiswahili akiungwa mkono na Mheshimiwa Spika wa Bunge. Kwa ujumla mheshimiwa Waziri na Spika wa Bunge kwa pamoja wameonyesha umuhimu wa Serikali na asasi zake kudumisha utamaduni wa kutumia lugha ya Kiswahili katika fomu na shughuli zote rasmi pamoja na mawasiliano yote ya Kiserikali. Wakati hayo yakiendelea, ni muhimu Wanazuoni na wadau wote wa lugha ya Kiswahili tuungane na Serikali katika kuondokana na dhana la kuwekeza kwenye maendeleo ya lugha za kigeni. Asasi za maendeleo ya lugha ya Kiswahili ziongeze uhamasishaji wa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika maeneo yote muhimu yaliyotajwa na mheshimiwa waziri na media zote ziachane na kabisa na matumizi ya 'KISWANGEREZA' katika utendaji wao wa kila siku. Wenu kwa staha; Ray Ephraim Ndewingiya Njau Mdau na mtetezi wa Kiswahili Dar es Salaam, Tanzania. Commentschega 20/04/2010 10:42am
Heko waheshimiwa,
Reply
Kambarangwe Sosthenes Kamanzi 22/04/2010 4:12am
Mimi nimefurahishwa sana na kitendo cha kurudisha Kiswahili chetu. tusiwe watumwa wa lugha za kigeni kwa sababu ya mgogo wa utandawazi.Wakija wajifunze lugha yetu.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA KISWAHILI CHETU.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed