Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete alifungua harambee ya kuchangia fedha uchaguzi mkuu CCM mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Harambee hiyo ilichangisha jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni Mia Mbili (200, 000, 000/-). YATOKANAYO Ni mengi. Nimeshindwa niandike lipi na lipi niache. Tafakari wewe! Comments15/05/2010 1:36pm
Kuchangia chama kweli ni muhimu, lakini kwa nini hatutaki kabisa kukubaliana na ukweli kuwa huduma za jamii na usimamizi wa malengo yetu mazuri ya maendeleo ndio kipaumbele cha muhimu zaidi kuliko mamilioni yote haya kwenda kwenye ustawi wa chama huku tukiacha hospitali zetu bila panado wala amoxiciline wala wakunga wasaidizi, tunaacha shule za msingi zisizo na madawati, chaki, vitabu vya kiada na walimu wenye njaa, ama ndio maana hatujengi vyoo madhubuti shuleni.. Vipi kuhusu kipindupindu kisichokwisha pale buguruni, kinoondoni moscow na mwananyamala?/aahh! kweli ccm yajenga nchi
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed