Katibu wa CCM kata ya Isamilo, Mwanza auawa 14/05/2010
Katibu wa CCM kata ya Isamilo jijini Mwanza Bw. Bahati Stephano (49) ameuawa kwa kuchomwa kisu mara baada ya kuvamiwa ofisini kwake na kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Jumanne Oscar (30). Tukio hilo limetokea leo majira ya saa sita na nusu mchana mara baada ya kijana Jumanne Oscar kuvamia ofisi hizo na kumkuta katibu huyo na kisha kuzuka majibizano ya maneno ambayo yalisababisha kijana huyo kuchomoa kisu na kumchoma Katibu huyo upande wa kushoto wa kifua na kisha tumboni. Katibu huyo wa CCM kata ya Isamilo alifariki njiani wakati wakiwa anapelekwa katika Hospitali ya rufaa ya Bugando kwa huduma. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Bw. Simon Siro amesema mara baada ya kufanya ukatili huo kijana Jumanne Oscar alitoka ofisini humo akikimbia kuelekea Ziwani lakini kwa nguvu za Wananchi alikamatwa na kupelekwa katik kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi. Credit: Albert G. Sengo, Mwanza CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |




RSS Feed