Maalim Seif atangaza kugombea Urais Zanzibar 12/05/2010
![]() Seif Shariff Hamad - CUF Hekaheka za maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao zimeanza kushika kasi kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ambapo Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad ameweka bayana nia yake ya kuwania Urais wa serikali ya Mapinduzi Zanziabar ikiwa ni miezi mitano kabla ya kinyang’anyiro hicho kufanyika. Hii ni mara ya nne kwa Kiongozi huyo, pamoja na mwenyekiti wa CUF Taifa, Ibrahim Lipumba, ambaye naye ametangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwania nafasi hizo. Akitangaza azima yake hiyo mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dar Es Salaam, Maalim Seif amesema dhamira yake hiyo ni thabiti. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ametoa rai kwa tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar –ZEC- kuhakikisha kuwa wananchi wanapatiwa fursa ya kujiandikisha bila kuwekewa mizengwe. Aidha Mwenyekiti huyo wa CUF ametoa rai kwa wabunge kuhakikisha kuwa wanashiriki vema katika mchakato wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2010 – 2011 na kuhakikisha kuwa bajeti hiyo inakuwa bora na kuwa chachu ya maendeleo na ustawi wa wananchi. Habari kwa mujibu wa TBC CommentsKenny 12/05/2010 3:51pm
Mimi sitasema lolote kwa huyu mgombea Zanzibar, ni haki yake. Hata hivyo mara mbili mfululizo alishinda. CCM waalinyanganya tu kura zake.CCM igeni mfano wa Gordon Brown Uiengereza. Kama kura hazitoshi si vizuri kupokonya.
Reply
12/05/2010 6:59pm
Huwa nawaza kama hakuna mwingine katika upinzani anayeweza kugombea. Yaani alichoshindwa kukifanya mara tatu zilizopita ambacho atafanya sasa ni nini? Anyway.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed