TAARIFA/HABARI kwa njia ya MAANDISHI
Swali: Mbona sioni habari mpya hapa?
Jibu: Ili kuona habari mpya, tafadhali safisha 'cache' (bofya hapa kujua jinsi ya kufanya hivyo) ya kirambaza (browser) unachotumia na kisha fungua upya tovuti hii (reload). Ikiwa tatizo halijarekebika, pengine unahitaji pia kusafisha 'cookies' (bofya hapa kujiua namna ya kufanya hivyo). Usipofanya hivi, mara nyingi utaendelea kuona habari zile zile za siku zilizopita na kukosa mpya zilizoongezwa.
PICHA
Swali: Mbona picha ni ndogo? na hazina maelezo?
Jibu: Picha zote zinazoonekana kwa udogo (zilizoko kwenye viboksi) zimekusanywa ili kupunguza kula nafasi ya ukurasa hivyo unachotakiwa kufanya ni kubofya katika picha husika ili kuzikuza kwa muonekano mzuri zaidi. Chini ya kila picha kuna maneno ya 'NEXT' kumaanisha bofya hapo kuona picha inayofuatia au 'PREVIOUS' yaani bofya hapo ikiwa unataka kuona picha iliyotangulia.
Maelezo ya picha (ikiwa yapo) yatakuwa yameandikwa na kuonekana chini ya kila picha. Baadhi ya picha hazina maelezo kwa kuwa hayakutolewa katika vyanzo ya picha hizo, ama, imezuiwa kutoa maelezo ya picha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kiusalama, usiri, nk au pengine picha hizo zimetumika ili kufikisha ujumbe tu ujumbe kusudiwa katika habari lakini hazihusiki moja kwa moja na habari iliyoandikwa.
Picha nyingine zilizobakia zitakuwa na maelezo chini yake (ikiwa yanapatikana).
TAARIFA kwa njia ya SAUTI (AUDIO & VIDEO)
Swali: Mbona hakuna taarifa mpya hapa?
Jibu: Baadhi ya siku hazipo taarifa mpya kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Ni dhahiri kuwa hatuwezi kufanya kila kitu kwa kila anachotaka mtu. Mtuwie radhi kwani tovuti hii inaendeshwa kama 'hobby' na siyo ajira rasmi, hivyo yote yanayowekwa hapa ni kutokana na nafasi aliyonayo mhusika bila ya kushurutishwa na yeyote. Tunawasihi pia kutembelea tovuti na blogu nyingine ambazo zinaweza kuwa na habari au taarifa mpya ili kukidhi mahitaji hayo. Baadhi ya tovuti hizo zimeorodheshwa katika ukurasa wa BloguRafiki na Linki.
Swali: Mbona pleya hazionekani?
Jibu: Tafadhali bofya hapa kusoma maelezo kuhusiana na swali hili.
SHUKRANI za dhati ziwafikie
- Wasomaji na watembeleaji wa wavuti.com
- Wale wote wanaotutumia habari kwa njia yoyote ile na kutaka zishirikishwe wanajamii.
PONGEZI twazitoa kwa
- Wale wote waliofanikiwa kupata ajira au/na nafasi za ufadhili wa masomo kupitia wavuti.com
- Wale wote wanaotoa changamoto ya kuboresha masuala mbalimbali katika tovuti hii na pia kwa nchi yetu.
ZIADA
Ikiwa una swali, hoja, dukuduku ama lolote ambalo halijaguswa hapa, tafadhali tuandikie kupitia kisanduku cha maoni kwa kubofya maneno yanayosomeka, 'comment' yaliyopo juu ya 'post' hii au kupitia anwani pepe ya wavuti.wavuti@gmail.com au kwenye ukurasa wa 'Contact Us' nasi tutatoa ufafanuzi kila inapowezekana.


RSS Feed