
Kila mtu ajue sisi sio watazamaji bali ni mhusika mkuu katika maendeleo ya nchi yetu kwa hiyo kufeli au kufaulu yoyote kama haikugusi moja kwa moja basi ina mgusa ndugu yako au hata rafiki yako wa karibu.
Badala ya kubaki tukilia kutokana na tunayoyaona naomba tuamke na kuwa chachu ya maendeleo ya nchi yetu kwa kufanya unachopaswa kufanya kwa uaminifu, juhudi na maarifa mahali popote au ofisi yoyote ulipo. Kwa kufanya hivyi mwisho wa siku utakuwa na ujasiri wa kusema MIMI NILIJITAHIDI KWA KADIRI YA NGUVU NA UWEZO ALIO NIPATIA MUNGU na utakuwa hudaiwi. - Wangaeli (akichangia kuhusu Takwimu za Tanzania)


RSS Feed