Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Amani Abeid Karume, amekutana na mabalozi wapya pamoja na wale wanaoondoka katika nyadhifa zao za uwakilishi. Pichani ni Raisi Karume akizungumza na Bi Ruth Leano ambaye ni mwakilishi mpya wa UNICEF Zanzibar pamoja na Balozi mpya wa Norway nchini Bi Jorunn Maehlum ambao walitambulishwa rasmi katika Ikulu ya Zanzibar il hali walioagwa rasmi ni Francoes Rumesi aliyemaliza muda wake wa kazi kuiwakilisha UNICEF Zanzibar na Bahar Nabil Helmy aliyemaliza nafasi yake ya Ubalozi mdogo wa Misri nchini Zanzibar. Credits: Ramadhan Othman/Ikulu - Zanzibar via Ahmad Michuzi/Jiachie blog CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |









RSS Feed