Raisi Jakaya Kikwete amewasili mjini Kampala, Uganda, kwa kuhudhuria mkutano wa kwanza wa nchi wanachama wa Mkataba Ulioanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court - ICC).

Raisi aliondoka jana kuhudhuria mkutano huo kufuatia mwaliko wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, mkutano huo unaanza leo na utamalizika Juni 11, 2010. Rais Kikwete atarejea nyumbani punde baada ya ufunguzi. Mkutano huo utapitia na kufanya marekebisho ya mkataba ulioanzisha ICC na orodha ya makosa yaliyoorodheshwa chini ya mamlaka ya ICC, kwa lengo la kuongeza au kuyatolea ufafanuzi zaidi makosa hayo. ICC ina mamlaka ya kuhukumu makosa manne ya mauaji ya halaiki, mauaji wakati wa vita, mauaji dhidi ya binadamu na visa vya uchokozi (ambalo halijapata tafsiri inayokubalika kimataifa katika mkataba huo). Mkutano huo pia utafanya tathmini ya  shughuli za mahakama hiyo tangu ilipoanzishwa Agosti, 1998, mjini Rome, Italia na kupendekeza namna ya kuboresha shughuli zake.

Credit: Freddy Maro via Issa Michuzi bog (picha); Gazeti la Uhuru (taarifa).
 


Comments




Leave a Reply