|
|
Rais J.M. Kikwete emekutana na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa. Kikao hicho kimefanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam tarehe 30.5.2010. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (credit: Mroki Mroki) Commentsben 30/05/2010 09:03
Sijui nini kilizungumzwa ila fanikiri agenda hapa sio jambo jingine ni uchaguzi mkuu. Naona Rais anawaweka sawa ili apate ushindi katika uchaguzi ujao. Kama ni mambo ya wajibu wao wa kazi kwa wananchi, Rais alikuwa wapi siku zote asikutane nao? OK, wakuu wa mikoa, Fanyeni juu chini msimwangushe boss wenu aliyewapa huo ulaji, hata kwa kuiba kura sawa tu, ili ushindi wa kishindo upatikane tena! 30/05/2010 12:32
Dadangu. C. Makawa Junior-Arusha 31/05/2010 03:51
Wote hapo juu nimewasoma binafsi nina mtazamo tofauti kidogo nao kama ifuatavyo kwanza ngugu yangu ben ukweli ni kwamba Rais amewaita Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala kama kikao cha kawaida ambavyo amekuwa akifanya nao mara kwa mara katika kupeana maelekezo ya kawaida katika utendaji wa kazi pia hata Mheshimiwa rais kujua maendeleo elekezi kutoka katika mikoa yote hivyo namshauri Ndugu ben awe na mawazo mapana kidogo si lazima Rais amewaita kwa sababu ya uchaguzi tu. Nikirudi kwa ndugu yangu Dadangu Ukweli unahitaji kuelimishwa kuhusiana na umuhimu wa kuwepo na Wakuu wa Mikoa kama ukifikiri kwa haraka haraka kama wewe mtu yeyote anaweza kufikiri kama wewe nadhani naweza nikachukua fulsa ukipenda nikupatie elimu ambayo baada ya kuipata lazima utakuwa umeelewa na pia kuwa na fulsa ya kuwafundisha wote wenye mawazo kama yako pole sana. 31/05/2010 07:23
Ndg Makawa. Leave a Reply |