TID asema Hasheem Thabeet amempiga! 09/05/2010
Hizi habari za "watu maarufu nchini Tanzania" kutafautiana na hatimaye kuzuliana magomvi yanayoishia kupigana si nzuri hata kidogo. Tabia hii ni mbaya kabisa katika jamii kwani inaendeleza habari za visasi ambavyo siku zote si tija katika kujenga maisha. Yeyote anayedhani ugomvi ni mtajiwa mafanikio, sidhani kama anatofauti na mtu anayepokea ujira wa haramu na damu. Watu wanaofahamika zaidi katika jamii wanapoamua kufanya vibweka hadharani badala ya kuwa mfano bora, huwa wameiajisi heshima waliyotunukiwa na jamii husika, na hii ni dharau. Haifai hivi. Habari ifuatayo imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya TID (Top In Dar - mojawapo ya wanamuziki wa kizazi kipya - Bongo Fleva/Fleva) anayedai kupigwa na Hasheem Thabeet (Hashim Thabit - Mtanzania wa kwanza kufanikiwa kucheza ligi ya mpira wa kikapu al maaruf NBA huko nchini Marekani). TID anaandika: ![]() TID - Khalid Mohamed Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiwa naongea na simu na Hisbert kwa sauti ya juu maana kelele za muziki zilikua zinasumbua nikiwa nimesimama nje ya mlango wa kioo ghafla akatokea bwana HASHIM ambaye alikua counter akiongea na wakata ticket akaja nje na kunipiga bonge la mtama nikaaunga chini ya sakafu na kuzirai kwa dakika kadhaa,mabaunsa wakanibeba na kuniweka pembeni maana nilikua mlangoni,nilipozinduka nilisikia maumivu makali kwenye mabega,mkono wangu wa kulia na mguu ambao unafanya kutembea kwangu kwa taabu,nikaangalia mkononi simu yangu sikuiona tena,nikawauliza mabaunsa wake jamaa amekwenda wapi!wakadai ameondoka tayari...nikajikokota kuelekea kwenye gari yangu na kuelekea polisi kutoa taarifa niweze kupata matibabu,nilipofika nikaaandika statement nikapewa namba ya case CD/RB/6848/10 pia nikapatiwa PF3 nikaenda hospitali nikapata matibabu,sasa hivi niko kitandani siwezi kutembea vizuri,pia nitashindwa kuperfom kwenye harusi ambayo tayari nishalipwa pesa tayari.SWALI langu ni kwanini ameamua kunidhalilisha vile mbele ya CLUB na FANZ ambao nilikua nawatumbuiza?kwanini ameamua kuniharibia kazi yangu?kwanini ameamua kunipiga bila ya kumkosea?JE NI SAWA HIVI JAMANI....naona MACHOZI YANANITOKA SINA CHA KUMUELEZA MAMA YANGU. Tovuti ya G5Click inaandika: ...kwa habari ambazo zipo chini ya kapeti kitaa ni kua inavyosemakana ANNA ambae ni rafiki yake TID aliekua nae club billcanas ndio chanzo cha ungonvi huo baada ya dem kutaka kumsalimia HASHIM THABEET na TID kukerwa na tukio hilo na akamletea dharau flani ndio akaamua kumpiga... Comments09/05/2010 7:38pm
Reply
Mimi 10/05/2010 12:04am
Wote wawili TID na huyo tolu nawachukia sababu ya kuvaa Heleni. Watu wakubwa wazima halatu wanafanya mambo ya ovyo, tena ni watoto wa kiislamu.
Reply
mama 10/05/2010 2:07am
Pole TID Tema mate tukamchape Hasheem
Reply
richard kilongola 10/05/2010 11:51pm
Nathani tusimchukulie T.d kama ni mkorofi kwani hatakama sababu ni mwanamke Dunia ya leo si yakugombania mwanamke na kwa maelezo yalivyo hashim ndiye aliyeanza kumkafua mwezake huo si uugwana.
Reply
Shilungo 12/05/2010 6:49am
Mambo ya kijinga tu, TID mwenzako yupo juu, usimuonee wivu, na uache uchokozi.Acha kufuta bangi
Reply
maxima 13/05/2010 12:26am
WEWE TID UNAONYESHA JINSI GANI ULIVYO BWEGE KILA UGOMVI NI WEWE TU KWA NINI NENDA KAPIMWE AKILI ZAKO MWENZAKO DUDUBAYA SAHIZI KAJIREKEBISHA USHAURI JIUNGE NA FRANCIS CHEKO AU KEKO KWA KINA MATUMLA
Reply
msemakweli 14/05/2010 1:45am
Kimsingi matatizo yako kwa wote wawili, kwanza tuanze na thabit huyu jamaa ni mchezaji wa ligi ya NBA, tena clab muda wa saa kumi na moja sasa sijui alikuwa anauza sura hapo bilzzz tena mlangoni na yeye ni star hakupaswa kuwepo hapo kwa muda huo kutokana na hazi ya ustaa wake,kwa hiyo nadhani hashimu hakuwa na washauri wazu katika likizo yake ya kipindi hiki, sidhani kama wachezaji wa ligi ya NBA wakiwa likizo huwa likizo zao wanazitumia kuzunguka kwenye ma kalbu coz hashimu alipo kuwa hapa kabla ya kuondo alikuwa akizungu kwe kila kumbi za stare akifika tu utasikia ikisema hashimu in the hous, then ashimu anaka kama dakika kumi halafu anaondoka anaelekea kwenye kumbi nyingine,sasa kijana anatakiwa kuwa na washauri wazuri,sina hakika kama tid amemtolea maneno ya zarau ila hatakama aliongea pale walipokuwa hashim asingesiki,ila siunajua mabaunsa na wale wahudumu wanamkubali hashim coz ni super star wa kweli lazima wangesema chocho walicho sikia kutoka kwa tid, na ukizingatia rekod ya tid sio nzuri pamoja na tabia zakeeeee, hayo ndio ya MM MSEMAKWELI.
Reply
popo 15/05/2010 4:22pm
http://www.habaricom.com/media/1129/TID_ON_HASHEEM_THABEET_BEATDOWN/
Reply
Micmos 18/05/2010 3:54am
Siku zote unaelipa kisasi unaonekana ni mwenye kosa. Kama TID alitoa maneno ya kashfa kwa Hashim sidhani kwa uwelewa wangu kama kumpiga TID ilikua ni suluhisho. Kwani huko ni kuchochea tuu ugomvi usiokua na maana. Na kwanza kwa kiwango ambacho Hashim amefikia sio mtu wa kufanya tena hayo mambo yasiokua na heshima, huko ni kujidhalilisha yeye na professional yake. Mie nilitarajia Hashim kama super star ndo wakati wa kuonyesha utofauti wake yeye na wengine, sasa na yeye akijiingiza kwenye ugomvi wa kipuuzi kama huo sasa hapo u-super star upo wapi? Anajipotezea heshima kwenye jamii iliyoanza kumpa heshima na kumuona kumbe hana la kuiga. Sasa wataka watu wakishakua ma - super star ndo waanze kupiga wenzao?. Mimi ningetegemea Hashim angeachana na huo ugomvi na labda kama kilimkera sana alichofanyiwa angemuita TID pembeni kistaarabu na kumueleza, hapo kwa kweli angeheshimika na huyo TID naamini hata angeogopa na kumheshimu kuliko kumpiga, kupigana ni mambo ya kizamani sana, dunia ya sasa ukimpiga mwenzio unaonekana wewe tuu huna maana. TID na wewe sasa umezidi, ni mambo mengi sana yamekukuta, ni wakati wa kukaa chini na kutafakari mambo yote uliowahi kukutana nayo na kubadilisha mwenendo wa maisha yako. Manake sasa wote mwajiona mlishakaa vichwani kwa watu...angalieni..msije mkajikuta siku mpo miguu kwa watu hao hao wakawakanyaga.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |






RSS Feed