Hii ni TV ambayo UNAPASWA KULIPIA. Kipindi cha kutizama bure kilishakwisha. Unachotakiwa kufanya:

  1. Nenda tv4africa.com
  2. Pakua (download) pleya yao na Install Player kwenye tarakilishi (computer) yako
  3. Rudi  tv4africa.com kisha bofya sehemu yenye icon palikoandikwa "PayPal" halafu lipia (utatumiwa Name na Password)
  4. Fungua pleya halafu bofya TV unayotaka kutizama (utatakiwa kuweka ile Name na Password uliyopata baada ya kulipia ndipo TV itafunguka)

Ukiwa na swali lolote au ukitaka maelezo zaidi ama una dukuduku, usiulize hapa wavuti.com, haihusiki kwa lolote zaidi ya kutafuta habari na kukupasha. 

Wasiliana na wahusika wenyewe kupitia maelezo yao kwenye ukurasa wao wa "contact":

info@tv4africa.com
0049721857651
contribution mensuel 5 euros  
payable sur paypal :donate@tv4africa.com
 

----
Shukurani Monsignor Fabby kwa taarifa ya tv4africa!

Picture
 


Comments

fredrick
11/05/2010 13:23

Natoa shukrani kwa uongozi wa blog hii kutuwezesha kupata habari za nyumbani live kupitia ITv.
Ila Kwenye computer yangu nikifungua ITV inagomagoma sijafahamu tatizo laweza kuwa ni nini!!naomba naelekezo hapo!!

Reply
11/05/2010 16:58

Fredrick,
Kwa utatuzi wa tatizo na kwa lolote lile, tafadhali wasiliana na wenyewe tv4africa.com kupitia anwani waliyoacha kwenye ukurasa wao wa 'Contact '

info@tv4africa.com
0049721857651
contribution mensuel 5 euros
payable sur paypal :donate@tv4africa.com

Reply
Abdul
11/05/2010 19:34

Reception ni mbaya sana. Hata bure kuangalia pia ni ghali kwasababu reception no mbaya ile mbaya.

Reply
Bashir
11/05/2010 23:54

Hongera ITV BIG UP.

Reply
Moshiro
12/05/2010 02:31

Nimeijaribu kuiangalia ila quality yake sio nzuri hata kidogo, nadhani labda ipo kwenye majaribio ila bado hairidhishi.

Reply
yasinta
12/05/2010 05:20

Subi siwezi kuangalia kabisa bahati mbaya kwani nilikuwa na shauku kweli

Reply
Abdul
12/05/2010 12:30

Kumbe yale matatizo yalikuwa ni jana tu. Leo ITV inaonesha kama njaa. Oh this is great. Big UP ITV. Lakini msije mkaanza kutucharge. Unajua sisi wabongo tushazoea bule.

Reply
12/05/2010 12:40

@Abdul tehe, wewe, 'bure' alishakufa, hukuhudhuria mazishi yake? au japo matanga? nhe he. Mi leo ninaitizama muda mrefu sasa ipo clear kabisa, jana tu kuna nyakati nilikuwa napata viboksi boksi na crr crrr nyingi hadi nazima, ila leo mambo mswano. Sijui watatuachia hivi hadi lini kabla hawajaanza kutuchaji, mwe, nakunja 'ngudo' wasahau LOL.

@Yasinta, pole dada wala sina namna ya kusaidia zaidi ya nilivyoeleza hapo juu.

@Wengine wote mnaolalamika, poleni, fanyeni kupotezea tu kama vile haikuwepo.

Reply
nshala
12/05/2010 13:31

jana was poor, leo the reception is so great... nshala, in Hanover,NH

Reply
12/05/2010 13:45

Ni hatua nzuri inayohitaji kupongezwa ila kwa kuwa mara nyingi vitu vya bure huwa vina matatizo naona itakuwa ni vyema kama tutatakiwa moja kwa moja kulipia ili tuweze kupata huduma nzuri.
Naijaribu hii ya dezo naona ina michenguo

Reply
Abdul
12/05/2010 18:30

Da Subi,

Leo mchana ilikuwa safi ile mbaya. Lakini hivi sasa sauti imevamiwa na CNN nilipokuwa ninaangalia matangazo ya Aljazeera kutoka ITV. Sijui kama hawa CNN wanatufanyizia kusudi kwa kuona tunapata kwa hili dezo. Sasa hivi picha ni za Aljazeera lakini sauti ni ya CNN. Ama kweli bure yauwa.

Reply
Abdul
14/05/2010 18:45

Da Subi,

Ile bure ya ITV imekwisha!

Reply
14/05/2010 18:53

salaaaale, kweli Abdul?
Niko mbali huku siwezi kucheki sasa hivi ila nachukua maneno yako.
Doh, tulijisemea hapa, hawawezi kuiachia bure muda wote, kila kitu ni biashara. Eeeniwei, bure alishakufa. tehe!

Reply
fred
17/05/2010 11:37

ninapotaka kuunganisha inaniambia chanel locked niingize jina na namba ya siri hii nitaipata vipi naomba msaada

Reply
17/05/2010 14:30

@fred, unatakiwa kulipia. Nenda kwenye tovuti husika, bofya kifute cha 'donation' kisha lipia.
Ukiwa na tatizo wasiliana na wahusika wenyewe kwenye tovuti yao, sisi (wavuti.com) si wahusika, wenyewe tumepewa habari na Monsignor Fabby kuhusu hilo, yeye naye alipewa linki na rafiki... basi stori ni ndefu ila cha msingi, tovuti husika ina 'contact' info, wasiliana nao.

Reply
Lulu
17/05/2010 17:45

Nimejaribu kulog in ili nione kama naweza kulipia lakini lugha imekuja kijerumani na mimi ni maimuna wa hiyo lugha. Pili naogopa isije ukalipia ukakuta account yako inakombwa yote. Naona kama wanataka tuwatumie cheque nitatuma au Western union nitafanya hivyo naogopa.

Reply



Leave a Reply