TUCTA vs Serikali - an update 12/05/2010
Dondoo za hizi zinatokana na mkutano wa wawakilishi wa TUCTA na Serikali uliofanyika Jumamosi iliyopita: - Nyongeza ya kima cha chini ya sekta binafsi iliyotangazwa na Waziri Juma Kapuya imeshusha kiwango kilichotangazwa mwaka 2007. - TUCTA haijatoa tamko kuhusu mgomo kwani inasubiri kuisha kwa siku 21 ambazo kwa mujibu wa Sheria, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana anapaswa kutoa tamko la makubaliano yaliyofikiwa. Siku hizo zimeanza kuhesabiwa tangu kuisha kwa mkutano wa Mei 8. - TUCTA ilishirikiana na wanasheria wake kupitia upya tangazo la Waziri Kapuya na kubaini kuwa halikufuata taratibu za kisheria ambazo ni pamoja na kutowashirikisha wajumbe wa bodi ya mishahara ya kisekta. Mgaya (TUCTA) alitoa mfano kuwa kiwango cha kima cha chini cha mishahara cha sekta ya viwanda na biashara cha mwaka 2007 kilikuwa Sh 150,000, lakini katika tangazo la Waziri Kapuya kiwango hicho kimeshuka hadi Sh 80,000. Katika tangazo hilo jipya, Serikali pia imefuta baadhi ya marupurupu ya wafanyakazi wa sekta hiyo na nyingine, ikiwa ni pamoja na posho ya nyumba, chakula, likizo na usafiri. TUCTA iliitisha mgomo ikidai Serikali imekuwa ikipuuzia madai ya Wafanyakazi kwa muda mrefu ambayo ni pamoja na punguzo la kodi inayokatwa kwenye mishahara, kuboreshwa kwa mafao ya uzeeni yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii na nyongeza ya kima cha chini cha mishahara katika sekta zote. Soma zaidi habari nzima kwenye gazeti Mwananchi (bofya hapa). CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed