
Dolores Atwood alidai kunyanyaswa kijinsia na askofu Burke wakati alipokuwa padri huko Warri kusini mwa Nigera kwenye mji wa Niger Delta. Hata hivyo, amesema uhusiano wao ulianza mwaka 1989 alipokuwa miaka 40 na binti akiwa na umri wa miaka 21. Amesema kwenye taarifa yake," Nilijibu haraka iwezekanavyo kwamba sijawahi hata siku moja maishani mwangu kumnyanyasa mtoto kijinsia. Huu bado ni msimamo wangu. Huu ni ukweli." Askofu Burke pia alimwomba radhi Bi Atwood na kuomba msamaha katika vituo vyake vya kanisa huko Warri na Benin.
Kanisa hilo limesema limekubali kujiuzulu kwake ambapo pia limetaja jopo litakalochunguza udhalilishaji wa watoto uliofanywa na viongozi wa kikatoliki huko Ireland.
Source: bbc.co.uk/swahili


RSS Feed