Nia nzuri. Tatizo lugha; Swanglish matege! 01/06/2010
Nimefahamishwa, "hii GH ipo Ifakara, ni nzuri na huduma poa kabisa, ila kwa hiyo 'ICE' no comment". Wito wangu ni kuwa tujitahidi kuandika lugha mojawapo kwa ufasaha. Hata mgeni anayezungumza Kiingereza anatarajia kusoma Kiswahili fasaha ndipo aweze kutafsiri kwa kamusi aweze kupata maana kusudiwa. Ikiwa unaweza kuandika Kiingereza fasaha, basi fanya hivyo, la inashindikana, basi tafuta mtafsiri. Hiyo itaisaidia biashara yako kukua. Tujifunze kutokana na makosa haya na tuwasaidie wengine kurekebika. Comments01/06/2010 1:42pm
nikweli mimi sina mengi ila sisi watz wengi ni wabishi hatupendi kusaidiwa tukijifanya tupo sahihi, tuulizejambo tusilolijua ili twende sawa, good,
Reply
Ali Machano ( Diku) Mussa 02/06/2010 12:12am
yaaani hii ndio athari zakujitumikisha wenyewe, kwasababu kama alihisi anauelewa mzuri walugha ya kiingreza sawa angeandika mneno yote kwa lugha hiyo .
Reply
02/06/2010 1:06am
Hii athari tokezi ya Kiswangereza ambayo ni lugha inayoendelea kukua nchini Tanzania.
Reply
Issah - KIA 02/06/2010 2:24am
Hee! huwa wabishi haoo, ukimwambia atasema si umeelewa!? Nahili neno si yeye tu wengi nawasikia wakisema AISII badala ya AC. si mseme tu kiyoyozi!
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed