Watu wawili wamekufa na wengine kiasi cha 58 wameugua au wanaugua ugonjwa wa kuharisha na kutapika katika kiijiji cha Gomelo kilichopo katika kata ya Kisaki , tarafa ya Bwakila, Morogoro. (credit: Mdau wa Morogoro via Beda Msibe/Lukwangule blog) YATOKANAYO Katika hali kama hii, wa kubeba lawama ni wahudumu wa afya, wananchi, Serikali ya Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa, Wizara? Nasema wahudumu wa afya hasa Wauguzi kwani imezoeleka kuwa Muuguzi ndiye huyo huyo ahudumie wagonjwa na afanye shughuli nyingine zozote katika eneo la afya, ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa mazingira. Inawezekana kabisa kuwa jukumu hilo limekabidhiwa fani ya Uuguzi kwa kuwa uwezo wa kuajiri Idara ya Usafi ni mdogo. Lakini utekelezaji wake haumaanishi kuwa Muuguzi ndiyo anawajibika moja kwa moja kutenda yale yaliyo nje ya fani ya Uuguzi. Yaani inakuwa kana kwamba wenye taaluma ya usafi na mazingira hawapo. Ninawalaumu wauguzi wenyewe moja kwa moja kwani inadhihirisha kuwa hawafahamu jukumu lao kuu ni UUGUZI. Wengi hujifanyia kazi kwa mazoea tu na itokeapo yupo atakayehoji iweje Muuguzi ndiye ashike ufagio, tando la kuondolea buibui, keni la maji, shimo la taka, incinerator, ufunguo wa stoo, daftari la stoku, uagizaji vifaa... na kumhudumia mgonjwa kwa wakati - huyo atakiona cha mtema kuni! Ataitwa mkorofi na mshari, mpenda ukuu, mpenda kujilinganisha, asiye na utii nk nk. Mimi nasema hii ni kutokuwa na mwelekeo (lack of focus) na kujiona kuwa waweza kufanya kila kitu (multi-tasking) ambapo matokeo yake ni kutokutimiza kikamilifu shughuli yoyote kusudiwa ikiwemo ya kutoa huduma kwa mgonjwa (under-performance or lack of, all together). Mwaichanganya jamii nzima, kwani hamueleweki haswa jukumu lenu lipi kwa maana hata kuhudumia wagonjwa bado ni lawama debe! Nasema Wananchi kwani upo wito kwa wananchi kujisushulisha katika kuboresha mazingira ya huduma za kijamii mojawapo ikiwa ni katika Zahanati na vituo vya afya. Wananchi wanaweza kujitokeza ana kwa ana kwa shughuli hizo au kutoa kiasi fulani cha fedha au malipo yatakayokubalika kwa ujira wa yule atakayekuwa tayari kufanya kazi husika. Nasema Serikali ya Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Wizara kwani hizi ndizo ngazi za ufuatiliaji wa maeneo yanayotoa huduma katika jamii. Hizi ngazi za utendaji na ufuatiliaji zimewekwa kwa makududi kwa minajili ya kurekebishana na kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa. Uonapo hali kama hii, bila kujali kwamba ni sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu nk, basi fahamu fika kuwa upo uzembe mahali fulani katika ngazi ya utendaji na utekelezaji. Inashangaza kabisa kuona kwamba hakuna aliyewajibika wala anayewajibisha katika hili. Huku ni kufeli. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |







RSS Feed