Siku ya Jumapili, tarehe 9 Mei 2010 kipindi cha Njia Panda kilikuwa na mgeni Dk. Jumanne kutoka 'Medicinal Plant Open Academy' ambaye alizungumzia suala la jinsi ya kuandaa vyakula na lishe muafaka kwa ajili ya afya ya Mama na Mtoto kwa kutumia vyakula asilia.

Dk. Isaac Maro
Bofya kifute cha play usikilize rekodi ya kipindi hiki. Ili kupata rekodi nyingine za NjiaPanda, bofya neno 'Dk. Isaac Maro' kwenye category hapo kulia mwa ukurasa au kwenye ukurasa wa audio.
Kipindi cha Njia Panda kinachoendeshwa na Dk. Isaac Maro na kurushwa na Radio Clouds FM kila siku ya Jumapili muda wa saa nane mchana hadi kumi alasiri (8 mch. - 10 ala.) na kimekuwako hewani tangu mwaka 2001 na inakadiriwa huwafikia wasikilizaji wapatao milioni tatu na nusu waliopo ndani na nje ya Tanzania.