Picture
Prof. David Mwakyusa / Tanzania - Waziri wa Afya
Utaratibu wa watumishi wa vituo vya afya vya umma kufanya kazi katika Vituo binafsi

Mheshimiwa Spika, Wizara itaimarisha huduma binafsi katika hospitali za umma hasa Hospitali za Kanda kama zinavyotolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi 32 ya Mifupa Muhimbili. Wizara itahakikisha kwamba madaktari na wafanyakazi wengine katika vituo vya kutolea huduma za ya vya umma hawataruhusiwa kufanya kazi katika vituo vya kutolea huduma za afya za binafsi bila utaratibu. Pale ambapo mtaalamu atahitajika kwenda kutoa huduma ili kuokoa maisha ya mgonjwa kutoka pande zote mbili za umma na binafsi, itafanyika hivyo kwa makubaliano maalumu kati ya taasisi husika. Hata hivyo, wataalamu hawa watapewa fursa ya kuamua kubakia serikalini au kwenda kufanya kazi katika vituo binafsi vya kutolea huduma za afya. Utaratibu huu pia utawahusu wafanyakazi katika vituo vya afya na vyuo vya ustawi wa jamii.

UTAWALA NA UTUMISHI
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2010/11, Wizara itaendelea kutoa ajira kwa watumishi wa Kada mbalimbali. Wizara itaajiri wataalam 160 na kuwapandisha vyeo watumishi 576. Aidha, Wizara itawapangia wataalamu wapatao 7,000 wa kada za afya katika mamlaka mbalimbali za ajira. Vilevile, Wizara itaendelea kuboresha mfumo wake wa kuhifadhia kumbukumbu. Pia, Wizara itatoa mafunzo ya maadili kwa watumishi wake wanaotoa huduma katika hospitali na pia itaandaa mkakati wa kupambana na rushwa.

UNUNUZI NA UGAVI
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/11, Wizara itanunua pikipiki 400 kwa ajili ya kubebea wagonjwa ili kutekeleza Mpango wa Afya ya Mama na Mtoto. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itanunua mtambo wa kujenga Zahanati kwa gharama nafuu (Ultimate Building Machine – UBM).

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2009/10, katika mkakati wa kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi, Wizara ilikamilisha taratibu za ununuzi wa pikipiki maalum 400 kwa ajili ya wajawazito wanapopata rufaa. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau ilinunua radio call 40 na magari 12 ya kubebea wagonjwa na kusambaza katika Halmashauri za Karagwe, Kasulu, Kibondo, Kigoma, Nachingwea, Kisarawe, Liwale, Ngara, Rufiji, Chunya, Ileje na Sumbawanga.

Jipakulie nakala kwa ajili ya kusoma hotuba ya Waziri kwa kubofya maandishi yanayosema 'Download'

 


Comments




Leave a Reply