Neno sahihi ni 'communication' 17/06/2010
Kulingana na maelezo, huenda neno sahihi lilipaswa kuwa, Communication (English) Mawasiliano (Kiswahili). Hilo neno 'commucation' ingekuwa limeandikwa kwa kutumia tarakilishi tungesema, 'typos' (yaani bahati mbaya limeponyoka) sasa hapa pengine kosa lilitendeka kutokana na kukosekana umakini kwa mwandishi? au kutokuwepo uhakiki kwa mmiliki wa sehemu husika? ama wote walighafilika kutokana na kiwango cha elimu? Sasa hata wateja au marafiki nao hawawezi kukosoa japo kumsaidia mwenye biashara? Au mwenye bishara naye kichwa ngumu? Kwa maana wapo wafanya biashara wanaosema, 'acha tu wataelewa hivyo hivyo"... na huo ndiyo mwendelezo wa uharibifu na matumizi mabaya ya lugha, hasa lugha ngeni. CommentsDavid 18/06/2010 12:24am
Hapo kosa si la mmiliki na wala si sio kukosa umakinifu wa mwandishi,bali wachoraji wengi lugha inawapiga chenga.
Reply
Jerda 18/06/2010 1:50am
Ni kweli mwandishi na mmiliki hawakuwa makini.Kwani hata kama mwandishi au mchoraji hajui anachokiandika mmiliki angekuwa makini na kusoma alivyochorewa kwani kwa njia hii atapoteza wateja kwani hawatajua alichusudia na lengo lake ahalitatimia.UMAKINI NA ELIMU NI MUHIMU KWA WAHUSIKA.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed