Nukuu ya Leo toka mwa Mtanzania... 05/06/2010
Enyi vijana kumbukeni tahadhari kabla ya hatari jambo muhimu katika utendaji wenu wa kila siku. Mlinzi wa maisha yako ni wewe mwenyewe na kamwe usitegemee mtu mwigine akulindie nafsi yako. ![]() Kumbukeni kuwa kila mtu hulia mama yangu na yarabi nafsi yangu na siyo mama yetu wala yarabi nafsi zetu. Zoezeni dhamiri zenu ili ziwe na utambuzi wa yaliyo mema na mabaya ili mpate tahadhari kabla ya hatari. Tatizo kubwa lenu vijana ni ubishi wakati mnapopewa madokezo ya mapema kuhusu hatari zinazoyakabili maisha yenu ya kila siku. Intaneti umekuwa uga wa kusaka mapenzi chini ya upofu wa fikra na dhana ya kwenda na wakati huku malezi bora ya wazazi yakifumbiwa macho kwa kiasi kikubwa. Nakumbuka maneno ya mwanazuoni wa lugha ya Kiswahili wakati aliposema kwa majonzi makubwa: "KIZAZI CHA WAZEE KULEA WAJUKUU NA SIYO WAJUKUU KUWALEA WAZEE. - Ray Njau (kutoka katika mfululizo wa maoni katika ukurasa wa Facebook) | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed