|
|
Askari wa Jeshi la Polisi wamefanya doria kwenye pori la akiba la Selous (Selous Game Reserve) wakati wa operesheni "Kipepeo III" ya kuwasaka na kuwakamata majangili wanaouwa wanyama pori. Jumla ya bunduki 63 zilikamatwa na watuhumiwa 105 kutiwa mbaroni katika operesheni hiyo iliyoshirikisha askari wa Hifadhi ya Taifa, TANAPA, Jeshi la Polisi na Askari wa Selous. Operesheni hiyo iliahirishwa siku ya Jumatatu. credit: Hassan Mndeme/Jeshi la Polisi via Sufiani Mafoto blog CommentsLeave a Reply |