Sasa wakacheze wapi? 13/06/2010
Mara nyingi watu wazima wamekuwa wakisahau au kutokutambua umuhimu wa michezo kwa watoto. Imezoeleka kwa wazazi kuwakataza watoto wao kucheza kana kwamba michezo ni dhambi. Heko ni kwa wazazi na walezi wanaokataza watoto kutumia muda mwingi katika michezo na badala yake wakawasaidia kupanga ratiba ya kuweka uwiano kati ya michezo na shughuli nyingine za kawaida ikiwamo shunguli za kukamilisha maihitaji ya mwanadamu kama vile usafi, kilimo, biashara na kuzingatia masomo. Tatizo kubwa nililoliona hapa lipo katika kuwanyima kabisa nafasi ya michezo! Wapo watakaokejeli kuwa, 'yaani badala ya kujali kujenga nyumba unasema watoto wakacheze? we vipi, unataka wakalale wapi sasa wakishamaliza kucheza?' Nami ningependa kujibu swali kwa swali, tatizo lako la kutaka kuishi mjini na maeneo yaliyobanana isiwe adhabu kwa wanao wa kuwazaa. Ulitumwa kuwazaa ujewatesa kwa kuwanyima haki zao za michezo? Tumesahau kuwa katika maisha ya sasa ambayo ajira ni adimu, michezo nayo imekuwa sehemu ya ajira. Hivyo kuwanyima watoto na vijana maeneo ya michezo ni kuwanyima uwezekano wa kupata ajira katika nyanja za michezo. Maisha ni kupanga, hujalazimishwa kung'anga'ania mjini. Wengi husema 'tutabanana hapa hapa' ndiyo penye 'dili' na maisha yanakwenda, lakini ikumbukwe pia kuwa hata wanaoishi nje ya mji maisha yanakwenda. Tukizaliana wengi, basi tuwe na mipango ya kutuwezesha kumudu mahitaji yetu. Tunang'ang'ania mahali pamoja ndiyo maana shughuli zote badala ya kupanuka kwenda kufuata makazi, watu wanapeleka makazi katika maeneo ya kazi. Hii ndiyo mojawapo ya matokeo ya msongamano barabarani. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed