Unaelewa nini hapa? Swanglish matege! 02/06/2010
Siyo utani, kejeli au kukebehi, ukweli ni kwamba sijaelewa maana ya tangazo hili. Kwa kuitizama picha napata wazo kwamba tangazo linahusiana na mikanda ya filamu inayoonekana hapo. Hivi kweli lugha ya Kiswahili imeshabadilika na kujaa maneno hivi? Haya maneno tafsiri yake inapatikana kirahisi kweli? Mlengwa katika lugha hii ni kijana wa kijiweni, Mtanzania, Mgeni au mtu gani hasa? Nadhani neno 'mtaharam' aliataka kuandika, 'mtaalamu' Je, neno 'kupwenti' alitaka kuandika, 'ku-point' ama neno hili tayari lina maana tafauti? Na neno 'muvu' ni Kuswahilisha neno la Kiingereza, 'move' ama maana kusudiwa ni nyingine? Pengine wakati mwingine mambo mengine yanahitaji kupuuziwa kwa kuwa 'hayanihusu', wale yanaowahusu watakuwa wameupata ujumbe. Tatizo nililo nalo, akiniuliza mtu mwingine maana ya ujumbe huo nitamjibu vipi? Pengine nitabaki tu kumwambia 'sijui' au 'nadhani' kama nilivyonyambulisha hapo juu, na pengine nitamweleza tu kuwa, 'kwa hilo, mimi kama wewe nimetoka kapa'. Mbaya zaidi ni ikiwa atakuwepo mgeni au mtalii akapekenyua kamusi yake na asione maneno hayo, kisha aniulize maana yake, pengine nitamjibu, 'lugha ya wahuni hiyo' au 'lugha nisiyoijua maana yake' na sidhani kama inawakilisha kabila lolote. Comments02/06/2010 9:41am
Nina wasiwasi kama ni kiswahili hiki. Duh!!
Reply
Subi 02/06/2010 10:45am
@Mzee,
Reply
Mtui 02/06/2010 10:27pm
Nakubaliana nawe dada Subi. Hii lugha ya Kiswahili inakuwa, na sababu vitu vingi tunatoa majuu (import) basi inabidi kubadili majina yale ya kiingereza kuwa kiswahili yakiwa vile vile.
Reply
Othman Michuzi 02/06/2010 10:28pm
Reply
02/06/2010 10:31pm
Jamani huyu jamaa alieandika hapa hajakosea wala nini,kwani hiyo yaweza kuwa ni lugha yao huko aliko.kwani kaka Mjengwa hii picha kaipigia wapi??? kama ni Iringa basi huyu jamaa yuko sawa kabisa maana wale hawawezi kutofautisha lafudhi na maandishi.
Reply
Issah - KIA 03/06/2010 2:10am
bwana mtui umekosea kidogo tu. huyu anamaanisha 'mtaalam wa ku-point movie' akiwa na maana kuwa yeye kila movie atakayoionesha ni kali kwa kuwa anapoint na si kuchua ilimradi movie tu
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed