Serikali imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani ili kuwezesha Wananchi wengi waweze kujisajili baada ya kusikiliza kilio chao cha kutaka muda zaidi wa kujisajili. Hayo yamesemwa Bungeni na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msollla wakati akiwasilisha hotuba ya makadrio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara hiyo. (sikiliza taarifa ya habari hapo chini kumsikia Waziri akitoa tamko hilo).

"Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu imesikia kilio cha wananchi wengi. Imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani hadi Julai 15, mwaka huu baada ya hapo simu zote ambazo hazijasajiliwa zitafungwa,” alisema Profesa Msolla.

Baada ya muda uliotengwa awali kuonesha kuwa watu wengi hawakuwa wamesajili laini zao, mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania, TCRA, iliongeza muda wa miezi sita, yaani Januari - Juni 30, 2010 kwa wananchi wote wenye simu kuwa wamesajili laini zao za simu kwa makampuni husika.

credit: Margareth Kinabo na Benjamin Sawe/Maelezo-Dodoma via: GPL
 


Comments

Mgoneke
30/06/2010 22:10

Mimi nadhani katika swala la usajili wa namba serekali haikuwa imejiandaa vya kutosha,kwani yapo maeneo mengi nchini ambayo ni vigumu kufikiwa na kusajili namba za simu kwa muda uliopangwa na kuwasilisha form za usajili mahali pale panapotakiwa form hizo kuingizwa kwenye rekodi.Matokeo yake ni kwamba utakutaka mtu amesajili zaidi ya miezi sita mpaka nane iliyopita lakini mpaka leo utakuta bado hajasajiliwa,sasa je yule mtu aliyepo kule zilipotoka zile form za usajili atwezaje kusajiliwa tena kwa muda huo wa siku 15 ulioongezwa?Utakuta labda hata form aliyosajilia ameipoteza,je huyo mtu atasaidiwa vipi?

Reply



Leave a Reply