"Those who cannot remember the past are condemned to repeat it. - George Santayana, who, in his Reason in Common Sense, The Life of Reason, Vol.1" au "Those who don't know history are destined to repeat it. - Edmund Burke (1729-1797)" kwa tafsrifi ya lugha yetu ni kuwa, "Watu wasioijua historia ni rahisi kurudia yaliyokwishapita", kwa maana kwamba, jamii inaweza kufanya mambo kwa kurudia rudia ili hali mambo hayo yalikwishatendeka siku zilizopita, matokeo yake ni kupoteza muda wa kusonga mbele au kusababisha madhara ambayo yangeweza kuepukwa ikiwa wangeifahamu historia. Tarehe 15 Machi 2009, mtengeneza filamu na msemaji katika masuala ya kijamii, Reggie Bullock alitoa filamu fupi kwa jina la "A War For Your Soul" ambayo ilitizamwa zaidi ya mara milioni sita ndani ya mwaka mmoja. ![]() Video hii ilitengenezwa ili kuwapa moyo vijana wa Marekani wa asili ya Afrika walio katika hatari ya kupotoka na kuvunjika moyo kutokana na matatizo wanayokumbana nayo katika jamii wanamoishi. Ndani ya video hiyo yumo mtu wa kufikirika kwa jina la 'Master of Darkness" ambaye anawakilisha taswira ya roho ya mtu mwovu mwenye nguvu ya kuingilia watu kiroho na kuwasababisha watende maovu juu yao na watu wengine. Filamu hii inaonesha kuwa "Master of Darkness" anatumia njia hii ya watu wa jamii fulani kuuana wenyewe kwa wenyewe. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, vijana wa kati ya umri wa miaka 14 - 17 ndiyo wanaoongoza katika mauaji haya. Ripoti za visa na matukio ya mauaji ya watu wa jamii ya Kiafrika kuuana wenyewe kwa wenyewe inaongezeka, kinyume na ilivyokuwa enzi za utumwa ambapo Mwafrika aliuawa na watu wasiokuwa Waafrika. video hii ikitumika vizuri itawasaidia vijana kuelewa historia yao na maovu waliyotendewa wazee wao na jinsi walivyopambana nayo hadi kufikia kupata uhuru wa heshima ya utu na ubinadamu na hivyo kutoa changamoto mahsusi katka kupambana na kurekebisha maisha ya sasa. Video hii imeshapokea sifa kemkem kutoka kwa mameya wa majiji mbalimbali, viongozi wa miji, vijana na vikundi mbalimbali vya kijamii duniani. Vijana wanapewa changamoto kushika hatamu katika kulea na kukuza vyema watoto wa leo ili kujenga taifa lililo bora. Video hii inaokenana katika ukurasa wa video (bofya hapa). CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed