Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk. Yohana Balele alikiri kufahamu kutokea kwa ajali hiyo na kwamba majeruhi walipelekwa katika hospitali za wilaya za Kahama na Bukombe kwa matibabu zaidi.
Abiria mmoja aliyesafiri na basi hilo na ambaye ni mfanyakazi wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Benjamini Jovin alizungumza na gazeti Mwananchi na kufahamisha kuwa, "Abiria wengi wamekufa, mimi nimeng'oka jino na kuumia mguu," alisema abiria huyo aliyelazwa kwa matibabu katika hospitali hiyo ya Kahama.
Baadhi ya watu waliokuwa kwenye basi hilo walisema kuwa magari yote yalikuwa kwenye mwendo mkali na na ndiyo sababu ya magari hayo kuharibika vibaya baada ya kugongana.
Hii ni ajali nyingine inatokea ndani ya mwezi mmoja kufuatia ajali nyingine zilizosababisha vifo vya makumi ya watu na majeruhi wengi zaidi.



RSS Feed