Azam FC yatangaza 22: Wapya 8, Waachwa 10 14/07/2010
Klabu ya soka nchini, Azam FC inayoshiriki ligi kuu soka ya VodaCom Tanzania Bara imetangaza usajili wa wachezaji ishirini na wawili, wanane kati yao wakiwa wapya huku kumi wa kikosi kilichopita wakiachwa. ![]() Said Mohammed Abeid / Mwenyekiti - Azam FC Katika taarifa iliyomo katika tovuti ya klabu hiyo, wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo ni Mohamed Binslum (Huru), Jackson Chove (JKT Ruvu), Jabir Aziz na Ramadhan Chombo 'Redondo' (Simba), Mrisho Ngasssa (Yanga), Kalimangonga Sam Daniel Ongala Rampling 'Kali Ongala' (GIF-Sweeden), Patrick Mutesa Mafisango (APR- Rwanda) na Peter Senyonjo (Polisi-Uganda). Wachezaji waliobaki ni John Bocco, Erasto Nyoni, Jamal Mnyate, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Vladmir Niyonkuru, Philip Alando, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Aggrey Morice, Salum Swed, Ibrahim Shikanda, Ally Manzi, Seleman Kasim 'Selembe' na Ibrahim Mwaipopo. Wachezaji waliopanda toka timu ya vijana 'Azam Academy' ni sita ambao ni Sino Augustino, Himid Mao, Mau Ali, Tumba Swed, Ali Mkuba na Samih Nuhu. Wachezaji walioachwa ni Chrispin Odula, Habib Mhina, Maridad Haule, Nsa Job, Said Swed, Salum Machaku, Yahya Tumbo, Ben Kalama, Shaaban Kisiga na Dan Wagaluka. CommentsKutoka katika papachi za moyo wangu naamua kabisa kutamka shikamoo kwa Said Mohammed Abeid kwa usimamizi wake mahiri na makini.Anachokifanya mzee Said ni kitu adimu sana katika soka la Tanzania na si kila mwenye macho anaweza kukiona wala si kila mwenye masikio anaweza kukiona ila acha wakati uamue na kila mdau wa soka atamtafuta mzee Said na kumpa mkono wa pongezi kwa shangwe,nderemo,vifijo na cherechereko.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed