"Update": Kwa mujibu ya taarifa ya Habari iliyosomwa saa mbili usiku na TBC1, ni watu 18 walionusurika kifo katika ajali ya Coaster iliyotokea majira ya saa nane mchana. Kamanda wa Polisi wa mkoa Maalumu wa Kipolisi Temeke, David Missime amesema hakuna yeyote aliyoepoteza uhai katika ajali hiyo. Dk. Asha Mahita wa hospitali ya Temeke amesema kuwa watu 13 waliojeruhiwa wamepatiwa matibabu katika hospitali ya Temeke na wengine 3 waliojeruhiwa vibaya wamepelewa katika Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. Basi aina ya Coaster lenye namba za usajili T 323 BEB linalofanya safari zake kati ya Mbagala na Buguruni limepata ajali mbaya baada ya kuanguka katika Mto Kizinga uliopo Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya abiria waliokuwa katika basi hilo wamejeruhiwa na inaripotiwa kuwa abiria watano wamefariki dunia katika ajali hiyo. Kwa habari na picha zaidi, tembelea GPL (credit) CommentsMr misalaba 20/07/2010 10:27pm
Tunachowaomba wtanzania na madereva wote , wawe makini tu wakati wanapo kuwa wakiendesha magari ,kwa mfano katika ajari iliyo tokea hii wapo watu baadhi wamepata ulema na wengine wamepoteza maisha yao na familia zao kupoteza matumaini ,baada ya kupoteza nguvu tegemezi.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |






RSS Feed