Dawa ya UKIMWI - huu ndiyo ukweli... 19/07/2010
Safari bado ni ndefu. Shamrashamra nyingi tulizisikia hivi karibuni pale watafiti wa NIH nchini Marekani walipotoa ripoti ambayo ni habari njema katika vita dhidi ya UKIMWI. Watafiti hawa wameeleza kuwa wamegundua chembechembe yaani antibodies, zenye uwezo mkubwa wa kuzuia virusi wa UKIMWI (HIV) kuingia kwenye seli nyeupe za damu — kwa 90% — na hivyo kusitisha mazaliano ya HIV. Pamoja na shamrashamra hizi, wengi wetu tukaanza kusikia habari potofu zikisambazwa na wanahabari Tanzania kuwa ‘Dawa ya UKIMWI yapatakana‘, na kusikia vijana wakianza kuongelea (labda kushangilia) ngono isiyo salama, πβ%ϕЖ&!! Ukweli ni kwamba ‘dawa ya UKIMWI´ haijagunduliwa - bali huu ni mwanzo tu wa safari ndeeefu ya kufikia nia hiyo. Mwaka jana kulikuwa na mlipuko wa habari kama huu kuhusiana na chanjo ya HIV – ila angalau ile ilikuwa tayari katika utafiti wa clinical trial! ‘Twisheni’ Bofya hapa kusoma 'twisheni'... NYONGEZA Mmiliki wa wavuti.com anakubaliana na kuafiki yaliyoandikwa na Joji/vijana.fm hapo juu kuwa, yali SAHIHI. Aina ya 'dawa' inayozungumziwa hapa ni antibodi ambayo watafiti waliipata kutoka kwa Mwanaume shoga mmoja Mmarekani-Mwafrika (African American gay man) ambayo ina uwezo wa kufisha ama kudhoofisha (neutralize) VVU (Virusi Vya UKIMWI). Watafiti hao walifanikiwa kupata antibodi ambazo walizipa majina ya VRC01 na VRC02. Antibodi hizi zimeweza kutumiwa katika maabara ya utafiti tu, (siyo katika mwili wa binadamu) ambapo zimeweza kufisha asilimia 91% ya aina mbalimbali ya virusi (neutralize 190 known HIV strains), huko nyuma, tafiti za awali zilishawahi kupata chanjo ambazo hazikuweza kufisha VVU kwa zaidi ya asilimia 40% ya "virus strains". Antibodi hizo huua VVU kwa kujishikiza katika sehemu kwenye mwili wa virusi na kuvizuia visibadilike hadi kufa (kwani kwa kawaida, virusi wa UKIMWI tabia yao ni kubadilika badilika na ndipo wakazaa "strains" tafauti). "The antibodies attach to a virtually unchanging part of the virus, and this explains why they can neutralize such an extraordinary range of HIV strains," Dr. John Mascola, one of the study's researchers said. Mtafiti husika na aliyehojiwa na kituo cha televisheni cha ABC (tizama video hapo chini) anasema, "bado itachukua MIAKA KADHAA kwa chanjo hii kutumika kwa wagonjwa wa UKIMWI na watu wanaoishi na VVU". "It's an important step in the right direction of adding a degree of precision to vaccine development," Dr. Anthony Fauci, director of the National Institute of Allergy and Infectious Diseases, told ABC News. "But there's no way to tell when a vaccine could happen." "We're going to be at this for a while," Gary Nabel, director of the center and a leader on this research, told The Wall Street Journal. Duniani hapa haijawahi kugundulika "DAWA" ya aina yoyote ile ya kuua Virusi moja kwa moja vikishakuwa katika mwili wa mwanadamu, isipokuwa, imewezekana kutengeneza chanjo dhidi ya Virusi wa magonjwa, kama vile chanjo za mafua, kupooza, kifaduro, dondakuu, nk. na kuwafisha au kuwadhoofisha virusi hao. Hadi sasa, tafiti za kisayansi zinasema UKIMWI-VVU husababishwa na Virusi. UKIMWI waweza kuababishwa pia na saratani, ujauzito, unyafuzi, kwashakoo nk, lakini uliosambaa ni UKIMWI utokanao na VVU (Virusi Vya UKIMWI), hivyo basi, ikiwa sayansi hii itaendelea kuwa sahihi, basi tutarajie kuwa kitakachopatikana kama 'dawa' ya UKIMWI kitakuwa katika orodha ya chanjo na si 'dawa'. Ufafanuzi wa neno 'dawa' Dawa ni neno linalobeba maana mbili au zaidi. Mosi, dawa kwa maana ya aina ya tembe au majimaji au ungaunga nk ambayo yaweza kutumika kuwaua vimelea vya magonjwa moja kwa moja; angalabu, huweza kutumika kuwafisha nguvu vimelea wa magonjwa kwa kuzuia uwezo wao wa kufanya kazi au kuzaliana. Pili, dawa kwa maana ya suluhisho la tatizo linalomkabili mtu au jamii. Kwa mfano, mtu anapokumbwa na tatizo akalitatua na kuweza kulipatia ufumbuzi, basi husema nimepata 'dawa' yake. ![]() Kwa hivyo, inapoandikwa 'dawa' ya UKIMWI, yawapasa watu wafahamu kuwa 'dawa' inayozungumziwa hapa ni mafanikio ya chanjo. Tusijisahaulishe kuwa mara zote tumekuwa tukiambiwa kuwa dawa ya UKIMWI tayari ipo, na nitairejea, 'Dawa ya UKIMWI ni kutokufanya tendo la ndoa', 'kuwa mwaminifu kwa mwenzi/mpenzi mmoja tu', 'wahudumu wa afya kuhakikisha wanachunguza vyema damu zinazoongezwa kwa wagonjwa ili kuwaepusha na damu zisizo salama', 'kuzingatia kanuni za kutokufanya yale yote yanayoweza kusababisha damu au majimaji ya mwilini ya mwenye VVU kukutana na damu au majimaji ya mwilini ya mtu mwingine', na njia kadha wa kadha. Natoa pole ya kipekee kwa makundi ya watu wanaoishi na VVU-UKIMWI waliopata kutoka kwa wazazi wao, waliobakwa, waliopata wakati wakitoa huduma kwa watu wenye VVU-UKIMWI kwa kujua ama kutokujua na makundi mengineyo. Sijatamka matumizi ya condom kwa kuwa hiyo siyo 'dawa' ya UKIMWI bali njia ya kusaidia kupunguza uwezekano wa kuupata maambukizi ya VVU kwa asilimia kubwa ikiwa itatumika inavyoelekezwa, nasisitiza kuwa 'dawa' pekee ni kwa kutokutumia condom kwa kufuata kanuni ya kwanza 'usijamiiane' hasa kwa wasio kwenye ndoa. Ikiwa ni lazima ujamiiane, basi uwe tayari kukubaliana na matokeo ya kujamiiana huko. (it is as simple as that). Kwa waliopo ndani ya ndoa, kuwa mwaminifu na acha kuwaka tamaa. Hakuna maneno ya kuremba wala haipo sababu ya kuuma uma kauli. Tatizo lililopo, 'hawataki kuambiwa ukweli ulio uchi' na wakiachwa bila kuambiwa, hulalamika 'kwa nini hamkutuambia' (damn if you do and damn if you don't). Taarifa utapewa, uamuzi utafanya mwenyewe, ili upate kukabiliana na matokeo ya maamuzi yako. Kisingizio cha 'sikufahamu' hakipo. Kwa wale Wakristo mtakumbuka maneno ya Mtume Yakobo katika kitabu chake sura 1:15, "tamaa ikichukua mimba, huzaa dhambi, halafu ile dhambi ikisha kukomaa, huzaa mauti'..., ndugu, utavuna upandacho!, lakini inavyoelekea, wanapanda wasipotegemea kisha wakati wa mavuno huduwaa na kuyakataa. Hiki si kipindi cha kuambiana maneno 'matamu' au 'yasiyo na uchungu' kwa kuwa VVU-UKIMWI hauzungumzi maneno matamu bali kuleta uchungu wa familia kufarakana, watu kuugua na kufa na kuacha utegemezi. ...na mavuno ya uzinzi, uasherati na ngono zembe ni mengi, yahitaji kurasa kadhaa kuyaorodhesha! References and more info: Commentsmdau 19/07/2010 3:21am
Excellent post!
Reply
Kusema ukweli, kama watu wangeweza, "blog visits highway" ingetakiwa ielekee hapa leo.
Reply
19/07/2010 6:59am
Subi infact ur the great especially in ur ellaboration using swahili.
Reply
JACKILINE 21/07/2010 2:18am
nimefurahi kupata hayo maelekezo yenu hivyo iliyopatikana ni chanjo na mbona vyombo vya habari tunavyo viamini kuwa ni chanjo moja wapo ya kutupa habari bado kinatupotosha asanten kwa kutuelewesha
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed