Ndiyo, ujumbe umefika, lakini, lugha imenyewa! Haifai kuwa hivi. Lipo tatizo kubwa kwa baadhi ya watu wa makabila fulani nchini Tanzania kuhusiana na matumizi ya herufi, 'R' na 'L' au 'H' na 'U' katika matamshi na hata kwenye maandishi. Pia, wapo wale ambao hushindwa kutofautisha kati ya herufi 'S' na 'Z' au 'P' na 'B' ama 'V' na 'F' na 'DH' na 'Z' na kadhalika. Ingawaje kwa maneno mengine huwa si rahisi kupoteza maana kusudiwa, makosa hayo bado huweza kuleta maana tofauti kabisa na iliyokusudiwa, hasa kwa mgeni au mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili. Kwa mfano, neno 'ukiri' ni tofauti na neno 'ukili' au 'karamu' na 'kalamu'. Vile vile 'kazi' ni tofauti na 'kasi' kama ilivyo 'vuma' ikawa tofauti na 'fuma'. Kadhalika, 'barua' ni tofauti na 'parua' ama 'dhana' na 'zana'. Matumizi yasiyo sahihi ya maneno hayo humlazimisha msomaji kujua maudhui ya habari kwanza ili kuweza kupata maana kusudiwa. Hii si vyema kwa wageni wanaojifunza lugha tunayojisifia kwayo kuwa ni asili yetu. CommentsBinaisa Rabisu 27/07/2010 1:44am
Watu wanaanza kama utani taratibu wanazoea.
Reply
Athuman 27/07/2010 2:14am
Safi sana kwa kutukumbusha. Kwa watanzania Kiswahili tunakirahisisha sana kwa kuwa tunajiona sisi ni waswahili na chochote tukiongeacho ni sawa, kumbe si sahihi. Hali hii uendelea hadi pale tunapoandika kwa kutumia kiswahili, ukisoma utagundua makosa mengi sana.
Reply
Alledros 28/07/2010 1:42am
Asante, ni kweli tupu, lakini vile vile majina ya watu kama Lobeti, Grolia, Raulenti, Kaloli, n.k. hasa hapa petu Iringa. Kwenye minibus fulani imeandikwa Cagrielo badala ya 'Cagliero', shule ya wasichana Ipogoro.
Reply
Issah 30/07/2010 4:03am
.....kazi kwelikweli!!!
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed