Ama kwa hakika picha hizi nikizilinganisha na makasri yaliyojengwa sasa, na jinsi wanavyochukua sheria katika kutetea na kuhalalisha ni kwa nini waishi katika makasri yenye thamani hiyo, ati "hali halisi hasa ya usalama kipindi cha sasa ikilinganishwa na nyakati za Mwalimu...", wingi wa maswali unazidi majibu! ![]() 'Hii ndiyo nyumba ya Mwalimu Nyerere aliyokuwa akifikia alipokuwa akisafiri kwenda Butiama akiwa kama Rais wa Tanzania kati ya miaka ya sitini hadi miaka ya themanini mwanzoni.' 'Ni nyumba ambayo ina vyumba vinne. Viongozi wenzake wa wakati huo walipomtembelea Butiama walistaajabishwa na udogo wa nyumba yake, na ndiyo wakafikia uamuzi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kumjengea nyumba nyingine kubwa zaidi ambayo ilijengwa miaka ya themanini katika eneo la Mwitongo. Ni nyumba ambayo ina vyumba vinne. Viongozi wenzake wa wakati huo walipomtembelea Butiama walistaajabishwa na udogo wa nyumba yake, na ndiyo wakafikia uamuzi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kumjengea nyumba nyingine kubwa zaidi ambayo ilijengwa miaka ya themanini katika eneo la Mwitongo.' - *Madaraka Nyerere. ![]() 'Hii ni nyumba ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) ilimjengea Mwalimu katika miaka ya themanini. Nyumba hii ilijengwa kwenye eneo la mwinuko la Mwitongo kijijini Butiama. Ni nyumba ambayo Mwalimu Nyerere aliishi kwa kipindi kirefu baada ya kustaafu uongozi wa Serikali akiwa kijijini Butiama. Msanifu wa jengo hili ni mwanamama ambaye jina lake sijaweza kulipata, ambaye aliandaa pia michoro ya hoteli maarufu ya Lobo iliyopo kwenye mbuga za hifadhi za Serengeti.' - *Madaraka Nyerere' Baada ya kwisha vita vya Kagera mwaka 1979, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliamua kumjengea Mwalimu Nyerere nyumba ya kuishi, ikiwa kama zawadi kwake kwa ushindi wa vita hivyo, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa wakati huo. Nyumba hiyo, ambayo ilijengwa Butiama ilijengwa na kitengo cha ujenzi cha JWTZ. Imejengwa katika eneo la Mwitongo, karibu na eneo ilipojengwa nyumba nyingine ya Mwalimu Nyerere aliyojengewa na Chama cha Mapinduzi. Ujenzi wa nyumba hii ulipoanza, wanajeshi walikatwa mishahara yao kuchangia gharama za ujenzi. Hata hivyo baadaye Serikali ya awamu ya pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi ilichukuwa jukumu la kuendeleza ujenzi ambao uliisha wakati wa Serikali ya awamu ya tatu ya Rais. Benjamin Mkapa, na kukabidhiwa kwa Mwalimu Nyerere mwaka 1999. Aliishi kwenye nyumba hiii kwa siku 14 tu kabla ya kwenda kwenye matibabu Uingereza ambako alifariki tarehe 14 Oktoba, 1999. - *Madaraka Nyerere ![]() 'Nyumba iliyojengwa kuzungukia kaburi la Mwalimu Nyerere, eneo la Mwitongo, Butiama.' 'Kabla ya kufariki, Mwalimu Nyerere alielekeza sehemu ambapo angependa kuzikwa, pembeni tu ya sehemu alipozaliwa. Haikuwezekana kumzika alipotamka kwa sababu ni sehemu ambayo ulijengwa mfereji wa maji machafu. Sehemu iliyochaguliwa baadaye haikuwa mbali na eneo aliloelekeza yeye.' - *Madaraka Nyerere' *Maelezo na Picha kama ilivyoainishwa, vimezipata kwenye blogu ya Madaraka Nyerere, mtoto wa Mwalimu. CommentsYasinta 18/07/2010 2:42pm
Nyumba ni nyumba tu hata kama ikiwa ndogo, lakini si yeye na familia waliweza kuishi. Watu bwana kwa vile alikuwa raisi basi ni lazima awe na lijumba likubwa la kifahari. Nimeipenda hiyo nyumba ya kwanza zaidi.
Reply
Niliwahi kufika butiama na kuingia ktk hiyo nyumba iliyojengwa kilimani (Mwitongo)miaka ya themanini nikiwa mdogo. Nyumba ina view nzuri.
Reply
eddy 19/07/2010 2:23am
Watu tusiwe na fikara mbovu nyumba ni nyumba tuu kwa wakati ule aliweza kujenga hivyo kwa sababu ya uwezo wake na aliiipenda chi hii ya ujama na kujitegmea na sema ujamaa na kijitegemea umeelewa hapo?sasa wakati huu tuliokuwa na ni wa ujamaa na kujimegea upo hapo?lazima kipindi hiki kiongozi ale na ajenge nyumba ya kifahari we kama huwezi kaa pembeni ari mpya na kasi zaidi
Reply
kamulinzi 19/07/2010 7:04am
Mwananch wa Kweli... Nani kama Kambarage Leo hii?
Reply
Mic 19/07/2010 7:52am
Mwalimu alikua anajali atakachoifanyia Tanzania na sio Tanzania itamfanyia nini...Ila viongozi wetu wa sasa wanajali Tanzania itawafanyia nini..na sio wao wataifanyia nini Tanzania kwa manufaa ya taifa letu. Uroho umeshawaponza viongozi wetu....
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |









RSS Feed