Hilo ni swali aliloliuliza kijiweni kwake juzi "mwananchi mimi" bloga Fadhy Mtanga. Swali lililotoa changamoto hasa kwetu ambao ni wapenda kufahamu mambo ili kupata ahueni ya kutokukaa 'Vilaza Room' muda wote. Kwa kuwa swali hilo halikupata majibu muafaka, na mimi nikiwa nishaingia "Vilaza Room" nikaona isiwe taabu, mguu mmoja hadi kijiweni Facebook, aidha nipate jawabu sahihi ama niongeze wafuasi 'Vilaza Room'. Maoni kadhaa yalitolewa na yalinifurahisha sana, mfano ni rafiki yangu Kalolo, yeye alichonifurahisha ni kwa kutokubali moja kwa moja kuingia 'Vilaza Room' bila ya kurusha ngumi kidogo, hivyo akajibu swali kwa kuuliza swali, ati, 'kuelekea wapi?'... Ama kabla ya hapo, alinifurahisha rafiki yangu Ng'wanambiti alipojibu katika blogu ya 'Mwananchi Mimi' kuwa inaanzia 'baharini'... sasa pamoja na 'umaimuna' wangu, nilishindwa kufahamu mwenzangu anagusia eneo lipi hasa la 'baharini' ndipo nikamwuliza mwenzetu wewe, "Kunduchi, Selander, Agha Khan, Feri, Bandarini, Kigamboni", wapi hasa? 'Schoolmate' wangu Chela pamoja na marafiki zangu wengine wa kijiji cha Facebook walijibu kuwa, inakoanzia sifuri ya umbali katika mkoa wa Dar Es Salaam ni katika Mnara wa Askari "Askari Monument", lakini saa chache baadaye kijiweni pale akafika 'schoolmate' wangu Carol, na 'uncle' Ray wakatukuta tupo katika gumzo na akina Kalolo, Abdala na Nico. Basi Carol na Ray wakatuasa, enyi wenye kutaka kupata ufahamu na kujua mambo, basi fahamuni ya kuwa, kwa hakika inakoanzia sifuri hii ni katika Mnara wa Saa, tena Carol akasisitiza kwa Kiinglish kabisa, "Clock Tower!!!"...! Majibu mawili yanajirudia sana hapa. Lazima moja kati ya hayo litakuwa ndilo jibu sahihi. Lakini unang'amua vipi usahihi wa jibu ikiwa huna si 'four table' ama 'past pepa' wala 'compass' la 'kugelezea' kujua jibu sahihi? Ndipo ikabidi kutumia ile kauli ya '...akili ya kuambiwa, changanya na yako...' nikakumbuka, ala, Baba ni Mhandisi Barabara, shida yote ya nini? Si "umtwange" swali hili akufahamishe katika upimaji wao wa barabara na mipango miji, kianzio au "center" huwa ni ipi? Yaani huanzia wapi kuihesabu hii sifuri? Sasa Baba naye akibanwa na shughuli, basi kusoma ujumbe kwenye barua pepe huwa si kipaumbele. Saa kadhaa zikapita bila majibu. Ilibidi 'nimkone' dogo Kevin aniulizie jibu 'fasta' hapo 'homu' maana niliona sasa pale kijiweni fesibuku karibu watu watatoana ng'eu. Basi jibu sahihi toka kwa Mhandishi wa Barabara na Mkazi wa Dar "ilipokuwa Dar kweli kweli enzi za Mwalimu", Engineer S. Tarimo akatoa 'fact' kuwa Kilometa sifuri katika Jiji la Dar Es Salaam inaanza kuhesabiwa katika MNARA WA SAA ndiyo CLOCK TOWER. Na ukweli ujulikane hivyo! Iweke hii katika kumbukumbu zako kwa faida yako na kizazi kijacho. Tusipoijua historia yetu na kuihifadhi, ni rahisi sana kubadilishwa na kupotoshwa. Imeandikwa hapa na itadumu hapa kwa urahisi wa kuirejea. Commentsmpekenyuzi 15/07/2010 7:33pm
hee kumbe kuna watu wasiolitambua hata hilo, bas hata kupiga vita ufisad itakuwa ngumu kama wameshindwa kujua vitu vidogo kama hivyo
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed