Kiswanglish matege: Both 'adullts'... 22/07/2010
Kusema, 'both adults & students' nadhani ni tafsiri ya moja kwa moja toka Kiswahili, haijakaa sawa. Mlinganisho uliotumika hapo ni wa makundi mawili ya nyanja mbili tafauti. Ni sahihi kulinganisha, 'Adults and Youths' au 'Students and Non-Students' kwa maana 'adult' akiingia darasani anakuwa 'student' vile vile 'student' anaweza kuwa 'adult'... namna gani vipi pale? Ipo haja ya wataalamu wa lugha kurekebisha haya. "Classes za Kiingereza..." yaani ni mwendo wa "ku-mix" lugha tu, haijalishi ni shuleni, mtaani, bungeni....!l Ukiuliza sana utajibiwa, 'lakini si umeelewa?' mmh! Wewe weka bango lako hivyo, kisha washindani waweke lao lililoandikwa kwa ufasaha, hapo ndipo utaelewa maana ya 'akili ya kuambiwa, changanya na yako...". Ndivyo tutakavyozungumza katika ushindani wa "Isti Afrikan Markiti"? 'ndo twaboronga hivyo halafu soko la pamoja likikolea, twakubali na kulalamika 'wenzetu wanatuzidi sisi hatujui chingereza', il hali wakati wa kukosoana kuwekana sawa, twaishia kuzodoana! Afanaleki! sisi ni sisi tu, chapa mfanowe "nehi". CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed