![]() Mwenyekiti mpya wa klabu ya soka ya Yanga, nchini Tanzania, Lloyd Nchunga amesema kuwa suala la kuanzisha kituo cha Radio na Runinga kwa klabu ya Yanga bado lipo palepale mara baada ya kukabidhiwa ofisi na viongozi waliomaliza muda wao, Nchunga amesema kuwa yapo mambo mengi ambayo yatafanyika katika klabu hiyo ili Yanga iweze kuwa na faida nayo. Mojawapo ya mambo hayo ni kukarabatiwa kwa kiwanja cha michezo kwa kushirikiana na mfadhali wa klabu hiyo ya Jangwani, Yusuf Manji. Kiwanja hicho kikishakarabatiwa kitatumika kwa mazoezi ya timu na siyo kwa michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara. credit: Jane John CommentsKEYE 21/07/2010 2:09am
pamoja na kwamba mimi si mpenzi wa Yanga ila hii hatua ni nzuri sana na inabidi kuungwa mkono na timu nyingine. Hii ni hatua kubwa ya maendeleo
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed