Kwa nini magonjwa ya mlipuko hayaishi? 21/07/2010
Huwa tunajiuliza ni kwa nini magonjwa ya mlipuko hayaishi jijini Dar na kwingineko mikoani. Watu wanaoishi maeneo kama yanayoonekana pichani huwa na kingamwili -immunity- ya hali ya juu dhidi ya magonjwa, ila miongoni mwao wapo 'carriers', yaani wale wanaobeba vimelea vya magonjwa mwilini mwao bila wao wenyewe kudhurika, lakini huwa chanzo cha kusambaza magonjwa na kuwaambukiza wasiokuwa na kinga na kusababisha kuugua. Hata hivyo, si magonjwa yote hujenga kingamwili. Njia pekee ya kujiepusha na magonjwa ni kwa kuzingatia misingi ya afya bora, ambapo msingi mkuu wa afya ni USAFI. Ni jukumu la Wananchi kuyafanyia usafi maeneo wanamoishi na kuzingatia kutotupa taka ovyo mitaani na barabarani, vile vile ni jukumu la viongozi wa Mtaa ambao ni wawakilishi wa Serikali ya nchi, kusimamia usafi wa mazingira na kuchukua hatua stahiki pale zinapokiukwa. Picha zinazoonekana hapa zimenaswa na kamera ya Francis Godwin alipokuwa akizuru jiji la Dar Es Salaam, Julai 2010. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |







RSS Feed