Wakati mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega akiwa katika majonzi makubwa ya kufiwa Baba yake mzee Ngezi, baadhi ya wagombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo wameamua kutumia msiba huo kwa kufanya kampeni za Ubunge, baadhi yao wakionyesha fomu zao za kuwania Ubunge makaburini hapo. Wagombea hao waliwashangaza watu wengi waliohudhuria shughuli za maziko hayo yaliofanyika katika makaburi ya Kitwiru mjini Iringa, kwa kitendo cha kila mmoja wao kuonekana akiwa katika jitihada za kujipitisha kwa wana CCM ambao baadhi yao ni wafiwa na kuomba kura. Jambo hili halijapata kutokea. Aidha, wagombe wengine waliamua "kujionesha" kwa kushika spedi kwa la kufukia mchanga katika kaburi hilo ili kuonekana kwa wapiga kura jinsi wanavyoshiriki bega kwa bega katika matatizo ya wananchi. Nina usemi niupendao sana, kuwa 'Siasa si hasa, bali visa na mikasa'! CommentsObserver 19/07/2010 10:36pm
Mbona hii imekaa kiumbeya zaidi. Sasa hata kushiriki kuzika nako asizike eti ataonekana anataka kugombea ?!!
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed