Karibu katika Mkutano wa Neno la Mungu ukifundishwa na Christopher Mwakasege - Reading, UK 23/07/2010
MKUTANO WA NENO LA MUNGU NA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE KUTOKA TANZANIA READING UK: 30 - 31 July na 01 August 2010 ![]() Jumuiya ya wakristo katika Uingereza na Ulaya inawakaribisha katika mkutano wa neno la Mungu utakokuwa ukiendeshwa na mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege kutoka Tanzania . Mwl. Mwakasege ni Mchumi na Mwalimu wa neno la Mungu ambaye mafundisho yake ni mapana na yanalenga katika maeneo yote ya maisha. MATARAJIO * Wenye shida za kiroho, nafsi, mwili mnakaribishwa mpate majibu ya maswali yenu. * Mafundisho ya namna ya kujikomboa kiuchumi kwa mujibu wa neno la Mungu yatafundishwa * Nyimbo za Injili kutoka wanamziki mbalimbali Huu utakuwa wakati wa baraka sana jitahidi usikose nafasi hii ya pekee na Mungu atakubariki. Anwani ya Ukumbi: Rivermead Complex Leisure Centre, Richfield Avenue, Reading, Berkshire, RG1 8EQ. Siku na muda wa mikutano: Ijumaa Julai 30 utaanza saa 8 mchana (2pm) hadi saa 2 jioni (8pm). Jumamosi na Jumapili utaanza saa 4 asubuhi (10am) mpaka saa 2 jioni (8pm). Kwa maelezo zaidi, wasilana na: Reading - 07888841971, Birmingham - 07776358464, London - 07817479845, Milton Keynes - 07787357618, Brighton - 07950324330 au 07944632826 / Rev, Emmanuel Chatawe - Mwenyekiti na 07776358464 Jackson Kapama - Katibu Mkuu. NYOTE MNAKARIBISHWA CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed