...huota, likamea na kuchanua, aidha likachumwa ama likafika mwishowe na kunyauka kisha hutoweka.

Hii ni picha iliyonigusa moyo wangu, ijapokuwa sifahamiani na yeyote katika picha hii, nafsi yangu imepatwa na huzuni kubwa. Nimetamani nijizuie lakini hisia nzito zilizojaa simanzi zimeshinda ujasiri wa nafsi. Ninajua Mungu ataweka njia kwa ajili ya malaika huyu aliyeachwa mikononi mwa mzazi mmoja. Yeye aliyeruhusu Mama kutangulia wakati huu alipohitajika zaidi kwa mwenza wake na mtoto wake, atafanya njia. Mipango yake si mipango yetu, mawazo yake si yetu, tukimtumaini na kumtegemea, atatuonesha njia. Yeye aliyeruhusu yote kutokea kwa kuwa Yeye ni Yeye, tukikubali ama kupinga, bado anabakia kuwa Yeye.

Ni kwa picha hii naguswa kuwaombea faraja wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki kifoni.

Mwenyezi, Yeye aliye mwingi wa rehema na neema, akupeni nguvu ya kutosha katika kipindi hiki kigumu.

Wimbo aliouimba Reuben Kigame na rafikize, 'Nitayainua Macho Yangu', uwe faraja kwenu nyote muaminio.
Picture
Enocent Mkindi, mume wa marehemu Jennifer akiwa na Mtoto wake, Collins Enocent (siku 3 tu) wakitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lililokuwa na mwili wa Jennifer Patric Mwela aliyefariki wakati akijifungua kwa njia ya operesheni katika hospitali ya Burhan Jijini Dar Es Salaam. Jennifer ambaye alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali TSN, upande wa mauzo alipumzishwa katika nyumba ya mielele kwenye makaburi ya Kinondoni.
credit: Yusuf Badi via Beda Msimbe/Lukwangule blog
 


Comments

31/07/2010 10:42

Subi, pole sana. Kimsingi nakubaliana na wewe kuhusu hili. Nakumbuka ilikuwa jana wakati naangalia picha ya mazishi ya dada mwingine mwandishi wa habari ambaye na yeye alifariki kwa matatizo ya uzazi. Machozi yalinidondoka kwa jinsi mumuwe alivyouaga mwili wa marehemu mkewe. Japo pia ni watu nisiowafahamu kabisa bali tu ni picha ya mazishi niliyoiona mtandaoni kwenye gazeti.

Reply
31/07/2010 11:16

Dada Subi - Asante kwa hili. Ni wakati kama huu ambapo imani za watu huweza kutikiswa na kudhorubishwa. Hebu mtazame huyu baba na kamalaika kake kachanga alikoachiwa. Mungu Ampe nguvu na kumfanya asonge mbele.

Mimi pia niliachwa na baba nikiwa mchanga sana na sikupata bahati ya kumwona wala kumfahamu. Lakini pengine nimekuwa hivi nilivyo kutokana na ukweli kwamba nililelewa na mama pekee ambaye naye alikuwa mgonjwa na mwenye upweke kule kijijini. Mipango ya Mungu imefichwa mbele yetu binadamu.

Mungu Amlaze marehemu pema peponi, Ampe nguvu mzazi huyu aliyebaki na akishushie mibaraka kimalaika chake kichanga. Kuna tumaini na jua la neema upeoni!

Reply
01/08/2010 00:37

Pole sana Prof. Masangu kwa kuondokewa na mzazi wako ungali mdogo. Mipango ya Mungu katika maisha yetu mingine kuitambua na kukubaliana nayo ni vigumu lakini apangacho huwa. Tumshukuru kwa yote.

@ Kaka Malkiory, Mungu atosha.

Binadamu tu maua, yote hapa duniani yatapita, ni kujilisha upepo. Heri wenye ridhiko na shukrani kwa Mola wao.

Reply
11/08/2010 04:56

Pole sana Subi kwa kweli huu msiba pia mimi umenigusa sana kwa kweli wakati naangalia hii picha na maelezo uliyoyatoa kwa kweli machozi yananitoka, fikiria wewe, mimi na wengine hatumfahamu (sio ndugu) lakini mtu unaguswa kihivyo sasa aliyeondokewa na mke ni aje, kwa kweli Bwana Yesu aendelee kumpa moyo wa uvumilivu wa hali ya juu. MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU.

Reply



Leave a Reply