Pichani ni Profesa Joseph Mbele ni Mhadhiri katika Idara ya lugha ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha St. Olaf kilichopo jimboni la Minnesota nchini Marekani ambaye alipata fursa ya kuhudhuria darasa la Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ambapo wanafunzi wa Shahada ya Juu ya Kiswahili walikuwa wakijadili wakijadili "utendi wa Hamziya", zaidi juu ya hudhurio hilo, bofya hapa kusoma posti fupi katika blogu yake. Profesa Mbele Amekuwa akialikwa kuzungumza katika vyuo, makongamano na warsha mbalimbali ndani na nje ya Marekani. Amekuwa akichagiza Wananchi kujenga tabia ya kupenda kujisomea vitabu na kujifunza mambo ili kuongeza ufahamu na kuweza kupata mbinu za kumudu na kukabiliana na maisha. Profesa pia amekuwa mstari wa mbele kabisa kupinga uvivu na kuendekeza starehe zisizo na tija maishani. wavuti.com inayo furaha ya pekee ya kufahamiana na kuendelea kushirikiana na Profesa Joseph Mbele. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed