
Sasa taarifa toka kituo kimoja cha redio huko barani Asia, 'Radio Free Asia' zinasema kwamba kufuatia matokeo hayo mabovu, timu nzima ya wachezaji pamoja na mejeja wao walihudhurishwa mbele ya umati wa viongozi wa Serikali wapatao 400, wanafunzi pamoja na waandishi katika ukumbi wa People's Palace of Culture na kuanza kupokea shutuma mfululizo kwa saa sita, toka Waziri wao wa Michezo Pak Myong-chol.
Wachezaji wawili wa timu hiyo Jong Tae-se na An Yong-hak, ambao wana asili ya Japan walikwepa aibu hiyo baada ya kuamua 'kutimkia' kwao ili kukwepa 'dhahama' ambayo walihisi ingewashukia.
Meneja wa timu hiyo, Kim Jong-hun amepewa adhabu ya kulazimishwa kufanya kazi ya ujenzi kwa kuwa kitendo cha timu kushindwa ilionekana ni usaliti wa moja kwa moja kkwa Kim Jong-un ambaye ni mtoto wa Raisi wa nchi hiyo, Kim Jong-il aliyekuwa akisimamia. Meneja huyo pia aliondolewa uanachama wake wa chama cha Wafanyakazi Wa Korea.
Inasemekana kuwa katika miaka iliyopita, iliposhindwa kufanya vyema katika mashindano hayo makubwa, timu nzima pamoja na kocha walikuwa wakiswekwa jela moja kwa moja bila utetezi wala kusomewa shitaka.



RSS Feed