Tukiwa tunahimizwa katika kauli mbiu ya Kilimo Kwanza, nimekuwa nikijiuliza ikiwa wakulima wanaohimizwa tayari wana mipango madhubuti ya kuuza au kuhifadhi mazao hayo punde msimu wa mavuno utakapowadia. ![]() Mkazi wa Kijiji cha Kipera Wilayani Mvomero mkoani Morogoro akiwa amepakia matenga ya nyanya katika pikipiki akiyapeleka sokoni kutoka shamba. Msimu wa mavuno wa zao la nyanya ambalo ni la biashara kwa wakazi wa Kipeara na vitongoji vyake umewadia lakini bei ya tenga moja la nyanya kama lililopakiwa katika pikipiki ni sh 3,000/= bei ambayo bado inaumiza wakulima. (credit: Mroki Mroki) Wasiwasi wangu ni kufanikisha dhana ya Kilimo Kwanza halafu mkulima ale hasara kwa kukosa soko litakalorejesha fedha ya mtaji na faida tarajiwa. Tunafahamu fika jinsi ilivyo taabu kupenyeza mazao ya chakula na maua katika nchi za nje hasa Ulaya. Sina uhakika tumeweza vipi hadi sasa kupenya katika masoko haya, hata na hivyo, mimi si mhusika wala mtaalamu wa nyanja hizo, hivyo siwezi kulisemea hili ama kinachonitia wasiwasi ni kuwa sijasikia wala kusoma taarifa za habari zinazoelezea jinsi Wakulima walivyonufaika na uuzaji mazao yao nje ya nchi. Ama pengine takwimu zake hadi kuzifuata katika Wizara, mashirika na taasisi fulani, kwa kuwa huu ndiyo mtindo uliozoeleka, yaani, kufanya tafiti na kuweka matokeo kwenye mafaili na kisha kuyafungia kwenye makabrasha na kuyaweka makabatini. Niendelee kuamini kuwa, pengine Kilimo Kwanza kitakuwa na kipaumbele katika mazao fulani tu, hasa mazao ya biashara ambayo huweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu. Natarajia kuwepo himizo na mkakati wa kuwasaidia Wanunuzi na Wafanyabiashara kujenga maghala muafaka ya kuhifadhia mazao. Natumai vile vile kuwa himizo litakuwepo kwa wenye mtaji wanaotaka kuanzisha viwanda vya kusindika malighafi ya mazao. Chonde chonde, yale tunayoyaona yakiyotokea mashambani na katika vituo vikuu vya mabasi kama vile Segera au Chalinze kwa matunda kuoza, yasigeuke kuwa janga la kitaifa la kauli mbiu ya Kilimo Kwanza. CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed