Tumewapoteza Waandishi wa Habari Wawili 26/07/2010
Wiki mbili hizi zimetawaliwa na simanzi baada ya kuwapoteza Wadau wa TEKNOHAMA nchini Tanzania. Tanzia ya kwanza ilikuwa la Bi. Hilda Mtenzi aliyekuwa mwandishi wa Habari wa kituo cha televisheni cha Taifa, TBC, ambaye alifariki katika hospitali ya Dk. Khan akiwa katika matibabu kufuatia maumivu ya ghafla ya kichwa. Bi. Mtenzi alikuwa akiiripotia TBC katika kituo cha Tanga, alikuwa mwenyeji wa Mbeya. Tanzia ya pili ni ya Bi. Primitiva Pankrasi, aliyekuwa mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi, ambaye amefariki katika hospitali ya Lugalo alikokuwa amefika kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa afya 'general check up' ambapo alipatwa na shinikizo la juu la damu 'high blood pressure' la ghafla na kufariki. Mungu azipumzishe pema roho za marehemu hawa na awape faraja wote walioguswa na misiba hii. AMEN. photo credits: Jane John na Muhidin Sufiani CommentsBinaisa 27/07/2010 1:40am
Wapumzike kwa amani.Poleni nyote mlioguswa na misiba hii
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed