Mtizamaji, shuhudia jinsi gari hilo, ambalo hakuna uhakika kama ni maalumu kwa uzoaji taka au la, lilivyojazwa taka kiasi cha kuziba vioo vyote anavyotakiwa kuvitumia dereva wakati akiendeshagari awapo barabarani. Tizama nafasi ya upana iliyochukuliwa na taka hizo ulinganishe na ukubwa wa bodi ya gari ufikiri dereva aliyeko nyuma na anayepishana naye pembeni anatakiwa kukadiria vipi ukubwa halisi wa gari hilo. Kwa mwendo huu kweli ajali za barabarani tunapambana nazo vilivyo au ni nadharia tu? Vikosi vya kusimamia na kuhakikisha uwepo wa usalama barabarani wangekuwa wanafanya kazi yao ipasavyo, huenda wazoa taka hawa wasingethubutu kujaza uchafu kwa kipimo hiki. Lau, wananchi tungekuwa tunajali afya zetu na kutii sheria, tusingekuwa tunafanya au kukubali mambo hatarishi hivi. Picha kama hizi pia za uvunjaji sheria kwa magari yanayozoa taka jijini Dar Es Salam, amekuwa akizipiga na kuziposti katika blogu yake bwana Othman Michuzi / Mtaa kwa Mtaa blog CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed