Raisi Mstaafu wa Tanzania awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa amezitaka nchi za Afrika kutoyumbishwa na propaganda za mataifa ya Magharibi kwamba wimbi la Wachina kuwekeza Afrika linaweza kuwafanya Waafrika kupoteza ardhi yao. Badala yake amezitaka nchi za Afrika kuweka mfumo mzuri wa majadiliano na Wachina, ili kushirikiana nao katika matumizi ya ardhi kwa lengo la kuzalisha kwa wingi na kukuza uchumi. ![]() Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa African Forum Dk. John Tesha mara baada ya kumaliza mkutano wa Maraisi wastaafu na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana uliokuwa unaelezea mikakati ya maboresho ya ardhi barani Afrika. (photo: Mroki Mroki) “Msije mkababaishwa kwamba wawekezaji Wachina wana lengo la kuwanyonya na kuwanyang’anya ardhi Waafrika. Kinachotakiwa ni mpango mzuri wa kujadiliana nao na kuweka mfumo mzuri kwa manufaa ya kiuchumi,” alisema Mkapa baada ya marais wastaafu wa nchi za Afrika kumaliza mkutano wao Jijini Dar es Salaam jana. Mkapa alikuwa akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari kuhusu propaganda zinazoenezwa na mataifa ya Magharibi ya kuzihadharisha nchi za Afrika kuwa Wachina wanaweza wakawanyonya na hata kuchukua ardhi yao. "Jambo la muhimu nchi za Afrika zinapaswa kuchunguza na kujua ni mwekezaji gani ambaye ana uwezo wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi haraka na kuwaletea wananchi maendeleo, na siyo kuangalia ni nani watashirikiana naye" alisema Mkapa. Akielezea mambo waliojadiliana kwenye mkutano huo, Rais Mstaafu wa Mauritus, Karl Offmann alisema suala la ardhi barani Afrika wameliona ni jambo nyeti ambalo linayumbishwa na misimamo mbalimbali ya kisiasa. Offmann alisema hawawezi kusema kwamba suala la ardhi Afrika halijatumika vizuri katika kuwaletea maendeleo Waafrika ila wana wasiwasi kasi ya ongezeko la watu, inaweza kuleta matatizo zaidi katika miaka ijayo. “Tunaposema idadi ya watu Afrika ni kubwa tunalinganisha na mabara mengine. Afrika imeonyesha kasi ya ongezeko la watu. Kwa mazingira hayo ni wazi matatizo yanaongezeka. Hali hiyo inaashiria kwamba sasa ni wakati wa kutatua matatizo yanayotokana na suala la umiliki wa ardhi,” alisema Offmann. Offmann alisema tatizo kubwa kwa nchi za Afrika ni kuweka usimamizi mzuri wa ardhi ni mawasiliano duni kama vile barabara na reli, hivyo masuala hayo, yanayopaswa kuwekewa kipaumbele. credit habari: Mwananchi Comments01/09/2010 3:46am
Mh.Mkapa kila hotuba zako huwa nazikubali sana,ni ukweli usiopingika kuwa una maoni na upeo mkubwa sana pia una nguvu za hoja wala huyumbishwi na mtu,hilo ndo linalokufanya kuwa kiongozi bora ingawa wengi nyumbani wanakubeza na kukukejeli.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |








RSS Feed