![]() Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume (kulia) akishiriki kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Augustino Ramadhani. Mkutano huo unaendelea katika Hotel ya Golden Tulip na unahudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania. Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani amewaonya wanasiasa wanaozungumzia kesi mbalimbali zilizopo mahakamani, katika majukwaa ya siasa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi. Jaji Ramadhani alitoa onyo juu ya kauli hizo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa semina ya siku tatu ya majaji wa mahakama za nchi 12 za Afrika. “Kesi zote zilizopo mahakamani hazitakiwi kuzungumziwa nje ya mahakama, mimi mwenyewe wakati kesi ya mgombea binafsi ilipokuwa mahakamani nilikuwa sitaki kuizungumzia nje ya mahakama,” alisema Jaji Ramadhani. Kuhusu hatua watakazochukuliwa watu wanaozungumzia kesi zinazoendelea mahamani, jaji Augustino alisema hawawezi kutoka mahakamani na kwenda kuwashika watu na kuwafungulia kesi bali mtu anatakiwa kupeleka malalamiko juu ya vitendo hivyo ndipo watakapoyafanyia kazi. Habari kamili ya semina ya siku tatu ya majaji wa mahakama wa nchi 12 za Afrika, isome katika Mwananchi CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed