John Mnyika anaiomba kura yako... 28/08/2010
CommentsMonsignor 28/08/2010 1:21pm
Go Mnyika go CHADEMA goo!
Reply
Mnyika John-miaka saba sasa tangu tufahamiane kama wapiganaji. Kwa namna ya pekee sana kila mmoja amefuata ndoto zake. Nakumbuka mwaka 2005 wakati upo kwenye hekaheka za kampeni dhidi ya Charles Keenja, siku ile tupo New Africa Hotel tulijadiliana kidogo kuhusu hali ya siasa jimboni Ubungo, sehemu kubwa ya majadiliano yetu ilikuwa ni wewe kujibu maswali yangu, nakumbuka nilikutwanga swali moja kuwa "umejiandaaje kupokea matokeo ya kushindwa uchaguzi hapo Ubungo", ukasema hutegemei kushindwa, tulibishana sana juu ya hili huku mimi nikitetea hoja yangu kuwa kushindwa ni sehemu ya matokeo hivyo huna budi kujiandaa na matokeo utayaoyapata. Mwisho wa majadiliano yetu tulikubali kutoautiana huku ukiniahidi kuwa ikiwa utashindwa basi utaenda mahakamani. Baada ya matokeo ya uchaguzi, kura zako hazikutimia na wala hukwenda mahakamani. Nilikupongeza kwani nilijua umekuwa lulu. Leo nimekuona ukiongelea kuongezeka kwa vipaumbele vyako toka vinne mpaka vinane. Ukweli ni kuwa John Mnyika unafanya vizuri sana,ni wazi umekomaa na unastahili kuingia bungeni mwaka huu. Naamini kwa sasa unajua sana na unaweza sio tu kupambana bali pia kuongoza kwa umakini. Nakutakia kila la kheri katika utumishi mtukuka wa umma wa mtanzania mnyonge.
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed