Mgombea mwenza wa Profesa Ibrahim Lipumba anayewania nafasi ya urais kupitia CUF, Haji Juma Duni ameponda utaratibu unaotumiwa na CHADEMA pamoja na CCM ambavyo vinawasafirisha wagombea wao wa nafasi ya urais kwenda kuomba kura kwa wananchi kwa kutumia usafiri wa Helikopta. Aliviponda hivyo wakati wa mkutano wa Chama hicho wa uzinduzi rasmi kampeni za ubunge na udiwani mkoani Kagera ulifanyika kwenye viwanja vya uhuru vilivyoko ndani ya Manispaa ya Bukoba. Akiwa ameongozana na mbunge wa viti maalumu wa chama hichu mkoani Kagera, Savelina Mwijage na wagombea wa nafasi mbalimbali za ubunge na udiwani akiwemo mwanasiasa machachari Feliciani, alisema mgombea anayeomba kura kwa wananchi kwa kupitia angani kamwe hawezi kuelewa matatizo na kero zinazowakabili wananchi walioko chini ya ardhi na namna ya kuzitatua. Duni alisema hatua ya vyama hivyo ya kuwapitisha wagombea wao angani badala ya kuwapitisha chini ya ardhi inadhihirisha wazi jinsi gani vyama hivyo wasivyowajali wananchi wanaowaomba kura za kuwapa ridhaa za kuwaingiza ikulu. Aliwaambia wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara kuwa kamwe CUF haitatumia utaratibu wa kuomba kura kwa kutumia helikopta, ijapokuwa CUF inao uwezo wa kuomba kura kwa kutumia helikopta. Aliendelea kusema kuwa CUF itaendelea kufanya kampeni zake kwa kutumia magari kwa kuwa matumizi ya magari yanakiwezesha chama hicho kitambue kwa urahisi kero na matatizo yanayawakabili wananchi,” ndugu wananchi huwezi kupitia angani ukaelewa kero zinazowakumba wananchi” alisema Duni. “Ndugu wananchi unapofanya kampeni kwa kupitia ardhini unapata uzoefu mkubwa sana, unaelewa kwa urahisi kero za barabara, unaweza kuelewa barabara zisizopitika na zinazopitika, wanaofanya kampeni kwa kupitia angani taarifa za kero zinazowakabili wananchi wanazisoma kwenye vitabu baada ya kuletewa”alisema mgombea huyo. Duni aliwaomba wananchi wakipe chama hicho ridhaa ya kuingia ikulu ili kiweze kutekeleza ilani yake vizuri, alisema ilani ya chama hicho inaeleweka na inaonyesha mwelekeo mzuri wa kuinua hali duni ya maisha waliyonayo Watanzania. Aliwaonya wananchi mkoani Kagera kuwa makini katika kuvichagua vyama vya kuongoza nchi, aliwaambia wasichague vyama ambavyo ni mali ya watu binafsi na ambavyo vinahubiri masuala ya udini na ukabila, alisema vyama hivyo ni hatari kwa maendeleo kwa kuwa vikiingia Ikulu vinaweza kufilisi nchi. “Kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaofikiri vyama wanavyoviongoza ni mali yao, ukitaka kuelewa vyama hivyo angalia viongozi hao wanavyoteuana, ikitokea nafasi mtu wa kwanza kufikiriwa lazima mjomba kwanza au shangazi au ndugu yoyote wa karibu na viongozi na wengine wanafikiriwa baadae, ndugu zangu kuweni makini na vyama hivyo msichague wagombnea wao” alimaliza. credit: Audax Mutiganzi, Bukoba via Michuzi post CommentsLeave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed