Juzi tuliona hapa picha za mradi wa maji uliofunguliwa eneo la Mchikichini wilayani Ilala jijini Dar Es Salaam.

Niliandika kuhusiana na ubaya wa kuwa na mipango mizuri ya mradi kwa ajili ya kuisaidia jamii, lakini kosa likatendeka katika kutokuwashirikisha walengwa, na matokeo yake ni wananchi kuona kama hawahusiki katika mradi huo, na hivyo kutokushiriki kikamilifu katika kuulinda, kuutunza na kuuendelea.

Picha inayoonekana hapa chini tena ni mojawapo ya mfano hai wa jinsi miradi isiyoshirikishi inavyoweza 'kususiwa' na kubaki kuwa kama urembo na magofu na kuishia kupewa majina ya kejeli.
Picture
Mfagizi wa soko la makumbusho jijini Dar es Salaam Bi. Mwajuma msaka akifanya usafi kwenye soko hilo hapo jana, soko hili limekua tupu (halina watu) kutokana na wauza vitu mbalimbali kulikimbia soko hili kwa madai ya kwamba hakuna biashara/Wateja. (photo: Robert Okanda)
Soko hili la Makumbusho ninalifahamu vizuri sana kutokana na kuwa karibu na makazi yetu. Nakumbuka wakati linajengwa na hadi kufunguliwa, nilikuwa nachekelea moyoni kuwa sasa walao kuna uchaguzi wa aidha kwenda sokoni Mwananyamala au Makumbusho (kutokana na kuwa nyumba ilikuwa eneo la kati ya masoko haya mawili), lakini cha kushangaza, soko la Mwananyamala liliendelea kubaki jeupe siku baada ya siku tangu kufunguliwa kwake. Nilisikitika sana. Ilikuwa ni mwaka 1996/97 na hadi leo hali ni iyo hiyo.

Nimeishi pia Ilala, nakumbuka Jiji walijenga soko kwa ajlii ya Wafanyabiashara wadogo wadogo ili waweze kuhama Mchikichini na Boma waelekee soko jipya, wakalazimisha na daladala kufanya 'ruti' zake eneo hilo. Lakini siku baada ya siku soko lilizidi kuwa 'jeupe' huku baadhi ya Wafanyabiashara wachache  waliohamisha makao na kufikisha bidhaa zao hapo wakilalamikia 'ukame' wa wateja, nao wateja wakilalamika 'umbali'.
 


Comments

mama vanessa
30/08/2010 04:40

poor vision+ poor planning= prove of failure

Reply



Leave a Reply