Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, amewachambua makada wa CHADEMA mmoja baada ya mwingine akiwemo Marando na Shibuda kwa akusema tuhuma zilizotolewa na CHADEMA ni matusi yasiyovumilika. Alisema, makada wote walioitukana CCM katika mkutano huo wa CHADEMA wapo katika kundi la watu wenye uelewa mdogo (Simple Mind People). ![]() Yufus Makamba / Katibu Mkuu CCM Kundi hilo ni miongoni mwa makundi matatu ya watu wenye uelewa na hivyo Makamba ana maana kwamba, viongozi wa Chadema wana akili ndogo. Aidha CCM imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutosubiri barua ya malalamiko wakati chama kinapokiuka mwongozo wa maadili kwa vyama vya siasa, ichukue hatua kukiwajibisha chama kinachokiuka makubaliano hayo. Makamba ambaye alikuwa akizungumza kwa ucheshi alisema amelazimika kulizungumza hilo kwa kuwa yeye binafsi hawezi kuvumilia kuona kiongozi wao akitukanwa. “Hata kama ingekuwa ni wewe, unaona baba au mama yako anatukanwa, ungevumilia? Hakuna anayeweza kufanya hivyo na kama yupo dunia itamshangaa, kuna uvumilivu wa kisiasa unaokulazimu uvumilie chama kinapoguswa lakini si huu,” alisema Makamba. Alitaja uvumilivu huo wa kisiasa kuwa ni kuvumilia pale chama pinzani kinapokukosoa katika masuala ya elimu, kilimo, huduma za jamii lakini si katika kejeli na matusi kwa kuwa yanakwenda kinyume na mwongozo wa maadili ya vyama vya siasa ambao kila chama kinapaswa kuufuata. Makamba akisoma baadhi ya makatazo ya mwongozo huo alisema chama chochote hakitakiwi kufanya fujo, vurugu, kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji au vitisho katika kampeni na kuongeza kuwa kinyume cha makatazo hayo, ndicho walichokifanya makada hao. Akimchambua kada John Shibuda, alisema, “eti (Shibuda) anasema CCM ni kama tairi bovu, sasa tujiulize, hivi tairi bovu ni nani kati yetu na yeye, Maswa (Jimbo alilokuwa akiliongoza kwa tiketi ya CCM) waligundua hili mapema, wakambwaga katika kura za maoni. “Kwanza baada ya kuona maji marefu, alikacha kugombea urais na kumsifia Kikwete kuwa ana maadili, anafaa tena akachangia Sh 200,000, leo anasema CCM gari bovu, kaishiwa hoja,” alisema. Kuhusu Marando alisema, “anapaswa amshukuru Kikwete, ninajua wenye kesi ya EPA si wakosaji bado ni watuhumiwa mpaka mwisho wa kesi, lakini hivi serikali ikamate watu hata kama ni tuhuma na wewe unawatetea, unatetea mafisadi?” Katibu huyo wa CCM alihoji kwa kuwa Dk Willibrod Slaa alishindwa kiapo cha kanisani cha upadri, hawezi kutunza kiapo cha kuongoza nchi. Amesema, hajali hata yeye (Makamba) akiwekwa katika kundi la wenye akili ndogo baada ya waandishi kuhoji kwa nini naye anazungumzia majina ya watu. source: TBC Commentsmagukuru ga ndulu 01/09/2010 8:58am
We makamba umeishiwa hoja, unatakiwa kujibu hoja zilizotolewa na viongozi wa chadema sio kutoa pumba, wewe ni kiongozi mkubwa wa chama na tulitegemea majibu ya kuwatetea hao viongozi wa ccm ikiwemo kukanusha tuhuma zote kwa hoja.
Reply
Babalao 01/09/2010 11:55am
Mbona Makamba haja-comment kwa Kikwete kushindwa kwenye suala la UFISADI kwamba kitu hiki kinam-disqualify kupewa urais? Je yeye anajiondoa katika grupu la hao "simple minded people" kwa kutoliona hili?
Reply
Tina 01/09/2010 9:52pm
Namshauri baba yetu malamba aache kuongea sana maana watanzania wengi wameshamuweka katika kundi fulani la watu,wanaozungumza mambo mengi ambayo......!nadhani busara ya mtu inajidhihirisha siyo kwa usema mengi ya hovyo bali ya maana kwa wote.
Reply
adam 01/09/2010 10:26pm
Tatizo Makamba hajui kuwa yeye ndiye anayemtukanisha 'baba yake'. Ansahau kwamba tatizo ni 'baba' kuwa UCHI mbele za watu.
Reply
Newton 01/09/2010 11:35pm
Makamba anatakiwa aeleze kama waliotajwa kweli hawahusiki na EPA awashawishi watu kuwa sio kweli tu la afungua madai mahakamani
Reply
Baba T 02/09/2010 3:10am
Alitaja uvumilivu huo wa kisiasa kuwa ni kuvumilia pale chama pinzani kinapokukosoa katika masuala ya elimu,kilimo, huduma za jamii......ina maana huyu mzee haoni lolote kuhusu rushwa!!!!!? Sishangai sana kwani huwa mara nyigi yeye husema halafu ndio anafikiri na sio kufikiri kabla ya kusema. Jamani Mbwa mzee hafundishwi mbinu mpyaa!
Reply
Juma A Juma 03/09/2010 2:22am
Maneno ya Yusufu Makamba yananiboa ile mbaya na iko siku nitampa live.. Sijui ni uzee unamsumbua... Maana hana point kabisaaa.. Ukituhumiwa unatakiwa ujibu tuhuma sio kuleta masihara na kejeli tena tuhuma zinazohusu maslahi ya wananchi!!!! Hawa wazee wamechoka tusiwalazie damu sasa hivi tuwaondoe walacheze na wajukuu zao majumbani mwao sio kejeli za kishamba kwenye maswala siriazi..
Reply
Leave a Reply | Vitabu vya WatanzaniaBofya picha ya kitabu unachokitaka ili ujinunulie nakala
Yaliyomo/CategoriesAll Hifadhi/ArchivesFebruary 2012 |





RSS Feed